DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Daniel Bendarugaho, amewataka askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan wakati wa uchaguzi. Amesisitiza kuwa jukumu lao ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya amani na utulivu.
Akizungumza Oktoba 8, 2025 katika ukumbi wa Polisi Jamii jijini Dodoma, ACP Bendarugaho amewakumbusha askari kuwa na ustahimilivu, kuheshimu maoni ya wananchi na kuhakikisha mazingira ya upigaji kura yanakuwa salama kwa wote.
Kwa upande wao, SP Isaya Muruke aliwakumbusha askari kutoruhusu kampeni siku ya kupiga kura kwa njia ya mavazi au kauli, huku ASP Mtuli akisisitiza umuhimu wa kusimamia usalama wa maeneo ya kupigia kura kwa kudhibiti msongamano na kuhakikisha vyombo vya moto vinapakiwa mbali na maeneo hayo ili kudumisha utulivu.