A
Anonymous
Guest
Sisi Wafanyakazi wa Ujenzi wa SGR kwa hapa Lot 1 ambayo inahusisha Dar – Moro baada ya kulalamika kuhusu Mkandarasi Mkuu, Yapi Merkezi kuwaondoa watu kazini kwa gia ya likizo huku wakiwa hawatulipi stahiki zetu ikiwemo, malipo ya NSSF, kumeibuka baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanatukamata kwamba kwa nini tunatoa siri.
Baada ya sisi kugoma kuanzia Jumatatu ya wiki hii (Septemba 2, 2024) tukishinikiza jamaa waingize fedha zetu tunazodai za NSSF, Idara ya HR ya Yapi inashirikiana na Polisi kutupa vitisho na kukamata watu ili mgomo uishe.
Mpaka muda tunaandika andiko hili wenzetu Tisa wameshakamatwa wakiwatuhumu makosa mbalimbali, wengine wamechukuliwa simu zao ili tu watunyamazishe.
Yapi wametoa tangazo kuwa hakuna atakayefukuzwa bila kulipwa haki yake, wamepandika hilo tangazo ubaoni ili tulione, ni jambo zuri lakini mbona upande wa pili wanataka kutunyamazisha?
Tunajua mradi umekamilika kwa asilimia kubwa na punguzo ni la kawaida, lakini kwa nini wasitupe chetu tumalizane vizuri?
Wafanyakazi wengi hatujaingizia makato ya NSSF tangu mwaka jana licha ya kuwa kila mwezi tunakatwa kwenye mshahara.
Tunatuma ujumbe huu kwa IGP, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na mama yetu Rais Samia Suluhu, watusaidie Mkandarasi atupe haki zetu ili tuachane kwa amani na sio kupeana vitisho na kuwakamata wenzetu.
Tangazo la Yapi baada ya sisi kugoma