Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Askofu Amani ameyasema hayo leo Julai 25, 2025 wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 100 ya Seminari ya Mtakatifu Yakobo Mtume iliyopo Kilema chini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaack Amani ametawaka Watanzania kuwa waangalifu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 na kuwachagua viongozi wenye maadili na si waliojaa tamaa na ulafi wa madaraka.
Askofu Amani ametoa wito huo leo Julai 25, 2025 wakati wa maadhimisho ya jubilei ya miaka 100 ya Seminari ya Mtakatifu Yakobo Mtume, iliyopo Kilema Chini, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika seminari hiyo na kuhudhuriwa na maaskofu, mapadri, waseminari wa zamani na wa sasa pamoja na waumini wa kanisa hilo.
Amesema: “Wanaojitoa sadaka, wanaojali haki, usawa, wanaojali wadogo, maendeleo ya wote, hao ndio viongozi wa ndani ya kanisa na nje ya kanisa, popote pale kiongozi anapoweka mahitaji ya raia mbele huyo ndiye anafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi.”
Kuhusu kusitishwa kwa misaada ya nje, Askofu Amani amesema nchi inapaswa kujimilikisha kutokana na utajiri uliopo na rasilimali zilizopo zinapaswa kugawanywa kwa usawa bila upendeleo.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi amesema kwa sasa baadhi ya Watanzania wamekumbwa na “ugonjwa wa uchu wa madaraka,” viongozi waliopo madarakani wakiendelea kupata manufaa binafsi, jambo ambalo amesema halimpendezi Mungu.
Pamoja na mambo mengine, Askofu Ruwa’ichi amesema miaka 100 tangu kuanzishwa kwa seminari hiyo mwaka 1925 imeweka historia kwa kutoa viongozi wa dini wenye weledi ndani ya kanisa hilo.

“Kristu alituonyeshea mifano ya utumishi kwa kujitoa nafsi. Tanzania ya leo tunapata shida sana kwa baadhi ya viongozi ambao dhamira njema inafutwa na ndio maana mali za umma zinaishia katika mifuko ambayo sio salama.
Na sasa kwa sababu ya uchaguzi tuangalie sana, wale wenye ulafi tusiwachague hao kabisa,” amesema Askofu Amani na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwachagua wale wanaojitoa kwa wengine bila ubaguzi na kujipendelea.
Amesema: “Wanaojitoa sadaka, wanaojali haki, usawa, wanaojali wadogo, maendeleo ya wote, hao ndio viongozi wa ndani ya kanisa na nje ya kanisa, popote pale kiongozi anapoweka mahitaji ya raia mbele huyo ndiye anafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi.”
Kuhusu kusitishwa kwa misaada ya nje, Askofu Amani amesema nchi inapaswa kujimilikisha kutokana na utajiri uliopo na rasilimali zilizopo zinapaswa kugawanywa kwa usawa bila upendeleo.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi amesema kwa sasa baadhi ya Watanzania wamekumbwa na “ugonjwa wa uchu wa madaraka,” viongozi waliopo madarakani wakiendelea kupata manufaa binafsi, jambo ambalo amesema halimpendezi Mungu.
“Tamanini utukufu ili tutambue maana ya ukuu, ukuu wa kweli ni utumishi, na fundisho hilo ni muhimu sana, sio mnauosikiliza hapa, bali kwa Watanzania wote ambao tumepatwa ugonjwa wa uchu wa madaraka.”
“Chawa wa kujikomba, wakujinadi, kujinyepezea kwa wale walio na madaraka kusudi ni sisi tupate kitu, hayo hatuyapokei popote, yanatupelekea kuona udhaifu wa utu wetu na tunampoteza mwelekeo mbele ya Mungu,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, Askofu Ruwa’ichi amesema miaka 100 tangu kuanzishwa kwa seminari hiyo mwaka 1925 imeweka historia kwa kutoa viongozi wa dini wenye weledi ndani ya kanisa hilo.
“Katika miaka 100, wamepitia vijana wengi hapa seminari hii, wamepata malezi, wakapata fursa ya kupambanua miito ya wito, wengine wakawa mapadri na wengine wakahudumu katika shuguli nyingine huku uraiani ambao tunawaona hapa uraiani,” amesema Askofu Ruwa’ichi.