Askofu awauliza wanaosema Maaskofu wanachanganya Dini na Siasa, kwani Waumini wanaishi hewani?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Askofu Musomba, akiwa kwenye homilia amehoji mambo mengi muhimu:

1. Amesema, zamani mtu akifariki watu walikuwa wanahuzunika na kulia sana, imekuwaje sasa, mtu anakufa, watu wanashangilia? Amesema lazima tujiulize ni nini kimetufikisha hapa? Nini chanzo cha haya? Lazima tuuseme ukweli, tusifanye mambo kwa ushabiki, tunaliharibu Taifa.

2. Askofu ameeleza kuwa tulikotoka kulikuwa kuzuri, kwa kuuzingatia ukweli, ilifikia mpaka wabunge waliweza kuwawajibisha viongozi wa Serikali, leo tuna bunge linaloitwa bunge la machawa, bunge lisilotetea ukweli.

Askofu amesema kuwa ni lazima tusimame katika ukweli, kwa sababu ukweli unaleta usalama, usalama unaleta umoja, umoja unaleta haki na amani. Ameendelea kueleza kuwa, kwa hali ya sasa, wakristo wamefikia hatua mpaka ya kubaguana kwa sababu ya vyama vya siasa, wanashindwa kumshuhufia Kristo aliye wa umoja.

3. Akinukuu kauli ya mwanafalsafa wa Kirumi, amesema mwanadamu amekuwa mbwa mwitu wa mwanadamu mwenzake kutokana na vitendo vyake ambavyo vimetengeneza dhambi ya jamii, na kwambi dhambi ya jamii imekuwa kubwa sana nchini mwetu. Ni lazima kila mkristo anajiulize anachangia vipi kwenye dhambi ya jamii, yaweza kuwa unabambikia watu kesi ili wanadamu wengine wateseke. Anasema kuwa, wapo watu wanaishi na kutenda kama vile Mungu hayupo, japo wamebatizwa.

4. Ameeleza kuwa siku hizi kuna kauli zinatoka eti viongozi wa dini mnachanganya dini na siasa. Amehoji je, ni wakati gani mtu anakuwa muumini wangu na wakati gani anakuwa mwanasiasa na siyo muumini? Kwani waumini wangu wanaishi angani? Je, muumini wangu akiwa mwanasiasa, na kupitia hiyo siasa naona amekengeuka na kuwa mwongo, amekuwa chawa, nimwache tu apotee, nisimwonye kuwa anatakiwa kuisji katika ukweli kwa sababu Kristo tunayemfuata anataka ukweli, haki na amani? Akamalizia kwa kusema kuwa yeye kama Askofu asipomwonya muumini anayeona anapotoka, ataulizwa siku ya mwisho, akasisitiza kuwa ni lazima kusimama katika ukweli.

NB: Askofu tunampongeza sana kwa homilia nzuri inayoishi, kwa maana mafundisho ni lazima yalenge maisha halisia ya waumini kila mmoja kwa kile ambacho anakifanya. Mwanasiasa muumini anatakiwa kuzingatia awe wa namna gani ili kupitia hiyo siasa atimize mapenzi ya Mungu, halikadhalika kwa mfanyabiashara, daktari, askari, mkulima, mwalimu, n.k. Kila mmoja pale alipo aishi katika ukweli na kutenda haki, na kwa kumfanya hivyo tutakuwa tunauishi upendo wa Kristo.

Screenshot_20260125-000726~2.png
 
Na Hawa makanjanja wa kilokole wanaojiita maaskofu nao wangekuwa wamenyooka, Majizi ya ccm yasingekuwa na sehemu ya kupumulia.
 
Asante baba askofu kwani umenifumbua macho naweza ona sasa, kumbe siasa na dini ni ndugu kwani watu wake ni waumimi na papo hapo ni wanasiasa.
Hoja hii itanifanya niulize hao wasiotaka dini kuwa siasa, na siasa kuwa dini wako wapi?
 
Aisee Askofu ka mwaga madini mengi mno..Na hii ndo dhana halisi ya ukombozi inakoanzia
 
Askofu Musomba, akiwa kwenye homilia amehoji mambo mengi muhimu:

1. Amesema, zamani mtu akifariki watu walikuwa wanahuzunika na kulia sana, imekuwaje sasa, mtu anakufa, watu wanashangilia? Amesema lazima tujiulize ni nini kimetufikisha hapa? Nini chanzo cha haya? Lazima tuuseme ukweli, tusifanye mambo kwa ushabiki, tunaliharibu Taifa.

2. Askofu ameeleza kuwa tulikotoka kulikuwa kuzuri, kwa kuuzingatia ukweli, ilifikia mpaka wabunge waliweza kuwawajibisha viongozi wa Serikali, leo tuna bunge linaloitwa bunge la machawa, bunge lisilotetea ukweli.

Askofu amesema kuwa ni lazima tusimame katika ukweli, kwa sababu ukweli unaleta usalama, usalama unaleta umoja, umoja unaleta haki na amani. Ameendelea kueleza kuwa, kwa hali ya sasa, wakristo wamefikia hatua mpaka ya kubaguana kwa sababu ya vyama vya siasa, wanashindwa kumshuhufia Kristo aliye wa umoja.

3. Akinukuu kauli ya mwanafalsafa wa Kirumi, amesema mwanadamu amekuwa mbwa mwitu wa mwanadamu mwenzake kutokana na vitendo vyake ambavyo vimetengeneza dhambi ya jamii, na kwambi dhambi ya jamii imekuwa kubwa sana nchini mwetu. Ni lazima kila mkristo anajiulize anachangia vipi kwenye dhambi ya jamii, yaweza kuwa unabambikia watu kesi ili wanadamu wengine wateseke. Anasema kuwa, wapo watu wanaishi na kutenda kama vile Mungu hayupo, japo wamebatizwa.

4. Ameeleza kuwa siku hizi kuna kauli zinatoka eti viongozi wa dini mnachanganya dini na siasa. Amehoji je, ni wakati gani mtu anakuwa muumini wangu na wakati gani anakuwa mwanasiasa na siyo muumini? Kwani waumini wangu wanaishi angani? Je, muumini wangu akiwa mwanasiasa, na kupitia hiyo siasa naona amekengeuka na kuwa mwongo, amekuwa chawa, nimwache tu apotee, nisimwonye kuwa anatakiwa kuisji katika ukweli kwa sababu Kristo tunayemfuata anataka ukweli, haki na amani? Akamalizia kwa kusema kuwa yeye kama Askofu asipomwonya muumini anayeona anapotoka, ataulizwa siku ya mwisho, akasisitiza kuwa ni lazima kusimama katika ukweli.

NB: Askofu tunampongeza sana kwa homilia nzuri inayoishi, kwa maana mafundisho ni lazima yalenge maisha halisia ya waumini kila mmoja kwa kile ambacho anakifanya. Mwanasiasa muumini anatakiwa kuzingatia awe wa namna gani ili kupitia hiyo siasa atimize mapenzi ya Mungu, halikadhalika kwa mfanyabiashara, daktari, askari, mkulima, mwalimu, n.k. Kila mmoja pale alipo aishi katika ukweli na kutenda haki, na kwa kumfanya hivyo tutakuwa tunauishi upendo wa Kristo.

Ni wazi neno la Mungu lemeelemewa na siasa, wahubiri waliwa siasa wakiwa madhabahuni
 
Ameeleza kuwa siku hizi kuna kauli zinatoka eti viongozi wa dini mnachanganya dini na siasa. Amehoji je, ni wakati gani mtu anakuwa muumini wangu na wakati gani anakuwa mwanasiasa na siyo muumini? Kwani waumini wangu wanaishi angani? Je, muumini wangu akiwa mwanasiasa, na kupitia hiyo siasa naona amekengeuka na kuwa mwongo, amekuwa chawa, nimwache tu apotee, nisimwonye kuwa anatakiwa kuisji katika ukweli kwa sababu Kristo tunayemfuata anataka ukweli, haki na amani? Akamalizia kwa kusema kuwa yeye kama Askofu asipomwonya muumini anayeona anapotoka, ataulizwa siku ya mwisho, akasisitiza kuwa ni lazima kusimama katika ukweli.
 
Na huo ndio ukweli usiopendwa na matapeli wanaopendwa kuitwa "viongozi".

Sasa wamekuja na hadaa ya "nyeti" kupotea.🙄
 
Back
Top Bottom