Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Askofu Dkt. Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe amesisitiza kuwa ajenda ya mageuzi ni mali ya taifa zima na haipaswi kumilikiwa na chama chochote cha siasa.
Akizungumza kuhusu mchango wa Rais Samia katika mageuzi ya taifa, Askofu Bagonza amesema kuwa taifa lilimfahamu zaidi Rais Samia kupitia Bunge la Katiba Mpya, ambako alionesha kipaji chake cha uongozi na mchango wake katika mchakato wa mageuzi ya utawala wa nchi.
"Ndiyo, alikuwa Waziri katika Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini hatukumjua. Kipawa chake kilionekana zaidi wakati wa Bunge la Katiba," alisema Bagonza.
Alieleza kuwa kupitia mjadala mpana wa Bunge hilo, taifa liliweza kuchambua historia yake, hali ya sasa, na mustakabali wake, na kwamba Samia alikuwa sehemu muhimu ya mjadala huo pamoja na marehemu Samwel Sitta.
Askofu Bagonza alisisitiza kuwa Rais Samia ni alama ya mageuzi na alipotangaza falsafa yake ya 4R, mojawapo ikiwa ni "Reforms" (Mageuzi), alikuwa anaendeleza msingi aliowahi kushiriki kuujenga. Hata hivyo, alieleza kuwa anatamani Rais Samia apige "flashback" ili kutathmini kile kilichomjenga na kuendelea kukiendeleza kwa maslahi ya taifa.
"Natamani hii ajenda angeichukua akaimiliki kwa kuwa alianzisha yeye, kuliko sasa imechukuliwa na hawa wapinzani wake wa CHADEMA ambao wanasema No Reforms, No Election," aliongeza.
Akihitimisha, Askofu Bagonza ametoa wito kwa Watanzania wote kuwa macho na kuhakikisha kuwa ajenda ya mageuzi haiwezi kumilikiwa na kundi fulani au chama fulani, bali inabaki kuwa ajenda ya kitaifa.
Amesisitiza kuwa mageuzi yalianza tangu awamu zilizopita na yalidhihirika zaidi katika awamu ya nne, ambayo ilisababisha kuundwa kwa Bunge la Katiba na kumfanya Rais Samia kufahamika zaidi kwa Watanzania