Askofu Bagonza amerudi tena. Sasa hivi anauliza "Mahakama imetupindua tuishtaki wapi?"

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Kuna haja ya kumlinda Askofu Bagonza kwa wivu mkubwa sana.

Jana kufuatia mwenendo wa Kesi ya Lissu, Askofu Bagonza ameshusha waraka mwingine kupitia ukurasa wake wa Facebook. Ameandika yafuatayo:

askofu bagonza.png

MAHAKAMA “IMETUPINDUA”: Tuishtaki wapi?

Bila kuathiri mwenendo wowote wa kesi isiyokuwepo au itakayokuwepo, najasirika kusema mahakama ya Hakimu Mkazi “imetupindua” katika kesi inayomkabili huyo “mpenda madaraka” Tundu Lisu.

1. Wananchi wa Tanzania (Jamhuri) tunamshtaki Tundu Lisu kwa tuhuma ya kutaka kupindua serikali yetu au kutupindua sisi.

2. Sisi Wananchi (Jamhuri) tumeandaa mashahidi wetu ili kuhakikisha tunamtia hatiani na kumnyonga. Tuna uhakika tutamtia hatiani kwa ushahidi tulio nao.

3. Sisi wananchi wa Tanzania (Jamhuri), kwa uzalendo tulio nao, tuko tayari kutoa ushahidi hadharani ili kila mtu ajue na hao wanaomtuma Tundu Lisu wajue kuwa tuko imara.

4. Tundu Lisu hashtakiwi na Rais wala na Jeshi la Polisi. Anashtakiwa na sisi wananchi wa Tanzania (Jamhuri).

5. Tunataka watu wote hasa chama cha Tundu Lisu, wajue kuwa Jamhuri yetu (wananchi) hatuna mchezo. Tutailinda nchi yetu kwa wivu mkubwa. Kesi hii iwe fundisho kwa wote wanaodiriki kuchezea mamlaka ya wananchi.

6. Ili hili fundisho liwe kamili, kesi hii tungetamani ifanyike uwanja wa taifa. Watu waone na kusikia. Na akipatikana na hatia anyongwe hadharani, siyo gerezani.

7. Kwa kuwa hata uhai wa jambazi ni muhimu utolewe kwa utaratibu, tunataka uhai wa wahaini wote utolewe kwa utaratibu na kwa uwazi. Sisi wananchi (Jamhuri) hatujamtuma yeyote kuficha chochote. Sisi ndio walalamikaji.

8. Wananchi (Jamhuri), wana haki ya kuhisi kuwa kuna njama za kutaka kumwachia Tundu Lisu pale wanapotaka kesi iendeshwe kwa kifichoficho na ushahidi utolewe kwa siri. Ipo hatari ya kuja kutuambia alitoroka!

9. Kwa kuwa mahakama ni yetu, serikali iliyotaka kupinduliwa si kwamba ni yetu tu bali serikali hiyo ni SISI wananchi, basi tuna haki ya kuhoji maamuzi yoyote yanayoweza kutaka kumtorosha huyu mtuhumiwa asiweze kuhukumiwa ipasavyo.

10. Kwa dalili za mahakama kutupokonya haki yetu ya kuhakikisha mhaini huyu anapata haki yake kwa uwazi, sisi wananchi (Jamhuri) tumeunda mahakama yetu ya wazi lakini iliyo vichwani mwetu, na itaendesha kesi hii na kuitolea maamuzi.

Tutafungua mashtaka ya “uhaini” dhidi ya mahakama iliyotupindua. Mwenyezi Mungu asipotusikiliza (Kitu ambacho huwa hakitokei), basi tutashtaki kwa shetani.

Sasa wananchi wataishtaki mahakama kwa kosa la kupindua mamlaka ya wananchi. Mashahidi wetu ni wa wazi na hakimu hapokei simu ya mtu yeyote. Mahakama jiandae.

MHAINI AKINYONGWA KWA HAKI, TAIFA LINASHANGILIA.

MAHAKAMA SIYO JANDO.
 
Ijumaa ijayo, nikienda kuswali, bagonza, lisu na watu wachache watakuwepo kwenye dua yangu.
Allah awape afya, moyo wa ujasiri na awalinde.

Maana viongozi toka dini yangu wengi wameamua kuwa wanafiki, wanaishi hata kinyume na maadili ya dini.
 
Kume-kucha 🔥

Fasihi nzito sana 😁😁😁

Kwa msio elewa Askofu anauliza kama Lissu ni mtuhumiwa wa uhaini Tafsiri yake ni kwamba kesi ya uhaini ni Ya Wananchi Kwa maana Serikali iliyopo madarakani iliwekwa madarakani na mamlaka ya Wananchi ,Hivyo basi Kuna sababu zipi za kujificha ficha hiyo kesi Hadi Wananchi wakose kujua kinacho endelea!?
 
Wakuu,

Kuna haja ya kumlinda Askofu Bagonza kwa wivu mkubwa sana.

Jana kufuatia mwenendo wa Kesi ya Lissu, Askofu Bagonza ameshusha waraka mwingine kupitia ukurasa wake wa Facebook. Ameandika yafuatayo:

View attachment 3446060

MAHAKAMA “IMETUPINDUA”: Tuishtaki wapi?

Bila kuathiri mwenendo wowote wa kesi isiyokuwepo au itakayokuwepo, najasirika kusema mahakama ya Hakimu Mkazi “imetupindua” katika kesi inayomkabili huyo “mpenda madaraka” Tundu Lisu.

1. Wananchi wa Tanzania (Jamhuri) tunamshtaki Tundu Lisu kwa tuhuma ya kutaka kupindua serikali yetu au kutupindua sisi.

2. Sisi Wananchi (Jamhuri) tumeandaa mashahidi wetu ili kuhakikisha tunamtia hatiani na kumnyonga. Tuna uhakika tutamtia hatiani kwa ushahidi tulio nao.

3. Sisi wananchi wa Tanzania (Jamhuri), kwa uzalendo tulio nao, tuko tayari kutoa ushahidi hadharani ili kila mtu ajue na hao wanaomtuma Tundu Lisu wajue kuwa tuko imara.

4. Tundu Lisu hashtakiwi na Rais wala na Jeshi la Polisi. Anashtakiwa na sisi wananchi wa Tanzania (Jamhuri).

5. Tunataka watu wote hasa chama cha Tundu Lisu, wajue kuwa Jamhuri yetu (wananchi) hatuna mchezo. Tutailinda nchi yetu kwa wivu mkubwa. Kesi hii iwe fundisho kwa wote wanaodiriki kuchezea mamlaka ya wananchi.

6. Ili hili fundisho liwe kamili, kesi hii tungetamani ifanyike uwanja wa taifa. Watu waone na kusikia. Na akipatikana na hatia anyongwe hadharani, siyo gerezani.

7. Kwa kuwa hata uhai wa jambazi ni muhimu utolewe kwa utaratibu, tunataka uhai wa wahaini wote utolewe kwa utaratibu na kwa uwazi. Sisi wananchi (Jamhuri) hatujamtuma yeyote kuficha chochote. Sisi ndio walalamikaji.

8. Wananchi (Jamhuri), wana haki ya kuhisi kuwa kuna njama za kutaka kumwachia Tundu Lisu pale wanapotaka kesi iendeshwe kwa kifichoficho na ushahidi utolewe kwa siri. Ipo hatari ya kuja kutuambia alitoroka!

9. Kwa kuwa mahakama ni yetu, serikali iliyotaka kupinduliwa si kwamba ni yetu tu bali serikali hiyo ni SISI wananchi, basi tuna haki ya kuhoji maamuzi yoyote yanayoweza kutaka kumtorosha huyu mtuhumiwa asiweze kuhukumiwa ipasavyo.

10. Kwa dalili za mahakama kutupokonya haki yetu ya kuhakikisha mhaini huyu anapata haki yake kwa uwazi, sisi wananchi (Jamhuri) tumeunda mahakama yetu ya wazi lakini iliyo vichwani mwetu, na itaendesha kesi hii na kuitolea maamuzi.

Tutafungua mashtaka ya “uhaini” dhidi ya mahakama iliyotupindua. Mwenyezi Mungu asipotusikiliza (Kitu ambacho huwa hakitokei), basi tutashtaki kwa shetani.

Sasa wananchi wataishtaki mahakama kwa kosa la kupindua mamlaka ya wananchi. Mashahidi wetu ni wa wazi na hakimu hapokei simu ya mtu yeyote. Mahakama jiandae.

MHAINI AKINYONGWA KWA HAKI, TAIFA LINASHANGILIA.

MAHAKAMA SIYO JANDO.
Kapiga local faint za hatari san, wenye akili wanaelewa vzr san hili andiko!! But machawa na snitches watabeza!!!
 
Back
Top Bottom