SI KWELI Askofu Bagonza amesema CHADEMA imefifisha matumaini ya Watanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1730393885651.png
 
Tunachokijua
Askofu Bagonza ni kiongozi maarufu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Zaidi ya kuwa kiongozi wa Dini Amekuwa akijihusisha sana na masuala ya kijamii na haki za binadamu nchini Tanzania. Mbali na majukumu yake ya kidini, Askofu Bagonza amekuwa akizungumzia mara kwa mara masuala ya kisiasa na kijamii, akisisitiza uwajibikaji, haki, na demokrasia.

Leo Oktoba 31, 2024 Mchungaji Peter Msigwa kupitia Akaunti yake ya Mtandao wa X amechapisha andiko lililoonekana kuwa ni la Jambo TV Tazama (hapa) lenye picha ya Askofu Bagonza pamoja na maneno CHADEMA IMEFIFISHA MATUMAINI YA WATANZANIA - ASKOFU BAGONZA

UPI UHALISIA WA TAARIFA HII?

JamiiCheck.com imefanya ufuatiliaji wa Mtandao na kubaini kuwa taarifa hiyo haijawahi kuchapishwa kwenye kurasa rasmi za Jambo TV kama linavyoonekana. Uchambuzi wetu umebaini kuwa Taarifa hiyo imezushwa na kufananishwa na machapisho ya Jambo TV ili kupotoshwa.

Aidha, Jambo TV kupitia kurasa zao rasmi wamejitokeza na kukanusha kuhusika na Taarifa hiyo. Katika kufafanua Jambo hilo wameandika:

Haya sio maudhui ya Jambotv_ , na hayako kwenye kurasa yoyote inayomilikiwa na JAMBO TELEVISION, sio sawa mtu wa kariba yako kushiriki hii michezo michafu inayoratibiwa na Chawa
1730394809380-png.3140017

Kanusho lililotolewa na Jambo TV​
IMG-20241031-WA0004.jpg

Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_________

Naona CHADEMA wanataka kwenda mashariki na magharibi kwa dakika ileile. Yaani wanataka kwenda mashariki wakati huo wanataka kwenda magharibi. Kwa kifupi hawajui waende wapi! Hawajui washiriki uchaguzi ambao hawajajiandaa nao au watie mpira kwapani kukwepa aibu na anguko kubwa? Kazi kwao kusuka au kunyoa.
Kwa ‘kuwashwawashwa’ kwangu nitumie fursa hii kwa nia njema, kuzungumza na ndugu zangu CHADEMA na Watanzania kwa haya yafuatayo:

1. Kama alivyosema Dk. Willbroad Slaa, CHADEMA imefifisha matumaini ya Watanzania kuona upinzani imara wa hoja za kuwaletea maendeleo. Kwa sasa CHADEMA imesinyaa na fikra za viongozi zimedumaa.

2. Kwa sasa Tanzania hakuna tena Chama Kikuu cha Upinzani. Tunaweza kusema tuna magenge ya wakuu wa upinzani. Hivi sasa tuna “kilichowahi kuwa Chama Kikuu cha Upinzani.” Kama nilivyosema tuna aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa (KKKT) na siyo Mkuu wa KKKT mstaafu.”

3. Kama CHADEMA kingekuwa Chama Kikuu cha Upinzani tusingeona ‘baridi yabisi’ ikimfunika Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu. Najua si lazima kuhudhuria kila tukio ili uonekane; pia si lazima kusema sana ili usikike. Lakini ukimya wa Mbowe na Lissu ni ishara CCM imejipanga vizuri kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tena kwa ile kauli yao kwa “Kishindo Kikuu.”CCM itashinda tena siyo ushindi wa patashika bali wa kishindo. CHADEMA haijui itie mpira kwapani au ishiriki uchaguzi. Muda utasema.

4. Uchaguzi ni mchakato siyo sawa na mbio za paka kukurupuka kwa kasi kisha anajificha nyuma ya mlango. Ukitaka kushinda uchaguzi lazima ujipange, uhamasishe wanachama wako na Watanzania wote kwani kura ni ushawishi. CHADEMA haijajiandaa wala haishawishi. Mbowe na Lissu wamepigwa na baridi yabisi.

5. Navipenda vya vya upinzani, lakini pia naipenda CCM kwa umakini na kujipanga katika kila uchaguzi. Sijatumwa na kanisa, CCM wala Rais Samia. Naweza kumpenda Rais Samia na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Lakini nasema ukweli CHADEMA haijajipanga na itapangwa na CCM katika uchaguzi wa Novemba 27.

6. Najua, mimi Bagonza ni Askofu wa wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama. CHADEMA msinitolee macho ninapowakosoa na CCM msishangilie mkabweteka kuacha siasa za kuwahudumia wananchi kama CHADEMA na wapinzani wengine walivyoacha kujali maslahi ya Watanzania. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa. Mbowe na Lissu wamepiga shoka moja mbuyu chini! CHADEMA chini!

7. Ni wazi Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongooza na kuizamisha CHADEMA. Ndiyo maana nasema tusimharibie. CCM imeonyesha uwezo kufunika upinzani kwa theluji nzito ya hoja na mipango mikakati mizuri kabla na baada ya uchaguzi.

8. Tuna tatizo kitaifa: CHADEMA hawajipangi kwa uchaguzi halafu ndio wakwanza kulia na kushika kichwa. CCM ikishinda tunasema hila kumbe hila ni za viongozi wa upinzani kushindwa kujipanga.

9. Mbowe na Lissu wakisema jambo mkawashangilia bila kuwahoji kwa hoja, mnawapa kiburi cha kusema bila kufikiri. Matokeo yake ni kama haya ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Vituo vingi mawakala ni wa CCM wa CHADEMA hakuna.Tunasahau nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari; si kuhemuka. Mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana. Wapimeni Mbowe na Lissu kwa maneno na vitendo vyao.

10. Mungu wetu analipenda Taifa hili, lakini Mungu hapendi uvivu wa kufikiri na ulaghai kila mara kulalamika wakati ametupa akili za kufikiri vema na kutenda kwa tija. Mbowe na Lissu wakiwa watu waliopewa fikra nzuri na Mungu wameshindwa kuzitumia na CHADEMA imezama kwenye tope la volcano wakati CCM ikichanua kwa mipango.

Usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili taifa. Kumbe CHADEMA ingeshinda Mbowe na Lissu wangetuzamisha. Mungu ana makusudi yake na CCM itaendelea kutawala kwa matakwa ya Mungu wetu.
 
View attachment 3140090

we na Lissu wangetuzamisha. Mungu ana makusudi yake na CCM itaendelea kutawala kwa matakwa ya Mungu wetu.
Huu utoto mlioedit mnapost kwenye kila mtandao wa kijamii ili mhalalishe wizi wa kura mnajidanganya. Bagonza hana utoto huu wa kuedit mabandiko yake.
 
Huyu ni Bagonza. Yeye na Dk. Slaa wameikosoa CHADEMA kwa hoja. CHADEMA ijisahihishe ukwli tuuseme hawakujiandaa kwa uchaguzi.🙏🙏🙏
 
Huu utoto mlioedit mnapost kwenye kila mtandao wa kijamii ili mhalalishe wizi wa kura mnajidanganya. Bagonza hana utoto huu wa kuedit mabandiko yake.
Naishia hapa, siendelei kusoma comments nyingine tena. Nilikuwa naitafuta comment kama hii, bahati nzuri nimeipata mwanzoni kabisa.

Askofu Bagonza hana lugha ya kishenzi namna hii.
 
..huu sio uandishi wa Askofu Bagonza.

..Askofu hana kawaida ya kuandika andiko refu kama hili.

..kama ana jambo lake anataka kulieleza basi atatumia maneno machache kufikisha ujumbe aliokusudia.
 
View attachment 3140090

Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_________

Naona CHADEMA wanataka kwenda mashariki na magharibi kwa dakika ileile. Yaani wanataka kwenda mashariki wakati huo wanataka kwenda magharibi. Kwa kifupi hawajui waende wapi! Hawajui washiriki uchaguzi ambao hawajajiandaa nao au watie mpira kwapani kukwepa aibu na anguko kubwa? Kazi kwao kusuka au kunyoa.
Kwa ‘kuwashwawashwa’ kwangu nitumie fursa hii kwa nia njema, kuzungumza na ndugu zangu CHADEMA na Watanzania kwa haya yafuatayo:

1. Kama alivyosema Dk. Willbroad Slaa, CHADEMA imefifisha matumaini ya Watanzania kuona upinzani imara wa hoja za kuwaletea maendeleo. Kwa sasa CHADEMA imesinyaa na fikra za viongozi zimedumaa.

2. Kwa sasa Tanzania hakuna tena Chama Kikuu cha Upinzani. Tunaweza kusema tuna magenge ya wakuu wa upinzani. Hivi sasa tuna “kilichowahi kuwa Chama Kikuu cha Upinzani.” Kama nilivyosema tuna aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa (KKKT) na siyo Mkuu wa KKKT mstaafu.”

3. Kama CHADEMA kingekuwa Chama Kikuu cha Upinzani tusingeona ‘baridi yabisi’ ikimfunika Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu. Najua si lazima kuhudhuria kila tukio ili uonekane; pia si lazima kusema sana ili usikike. Lakini ukimya wa Mbowe na Lissu ni ishara CCM imejipanga vizuri kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tena kwa ile kauli yao kwa “Kishindo Kikuu.”CCM itashinda tena siyo ushindi wa patashika bali wa kishindo. CHADEMA haijui itie mpira kwapani au ishiriki uchaguzi. Muda utasema.

4. Uchaguzi ni mchakato siyo sawa na mbio za paka kukurupuka kwa kasi kisha anajificha nyuma ya mlango. Ukitaka kushinda uchaguzi lazima ujipange, uhamasishe wanachama wako na Watanzania wote kwani kura ni ushawishi. CHADEMA haijajiandaa wala haishawishi. Mbowe na Lissu wamepigwa na baridi yabisi.

5. Navipenda vya vya upinzani, lakini pia naipenda CCM kwa umakini na kujipanga katika kila uchaguzi. Sijatumwa na kanisa, CCM wala Rais Samia. Naweza kumpenda Rais Samia na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Lakini nasema ukweli CHADEMA haijajipanga na itapangwa na CCM katika uchaguzi wa Novemba 27.

6. Najua, mimi Bagonza ni Askofu wa wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama. CHADEMA msinitolee macho ninapowakosoa na CCM msishangilie mkabweteka kuacha siasa za kuwahudumia wananchi kama CHADEMA na wapinzani wengine walivyoacha kujali maslahi ya Watanzania. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa. Mbowe na Lissu wamepiga shoka moja mbuyu chini! CHADEMA chini!

7. Ni wazi Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongooza na kuizamisha CHADEMA. Ndiyo maana nasema tusimharibie. CCM imeonyesha uwezo kufunika upinzani kwa theluji nzito ya hoja na mipango mikakati mizuri kabla na baada ya uchaguzi.

8. Tuna tatizo kitaifa: CHADEMA hawajipangi kwa uchaguzi halafu ndio wakwanza kulia na kushika kichwa. CCM ikishinda tunasema hila kumbe hila ni za viongozi wa upinzani kushindwa kujipanga.

9. Mbowe na Lissu wakisema jambo mkawashangilia bila kuwahoji kwa hoja, mnawapa kiburi cha kusema bila kufikiri. Matokeo yake ni kama haya ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Vituo vingi mawakala ni wa CCM wa CHADEMA hakuna.Tunasahau nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari; si kuhemuka. Mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana. Wapimeni Mbowe na Lissu kwa maneno na vitendo vyao.

10. Mungu wetu analipenda Taifa hili, lakini Mungu hapendi uvivu wa kufikiri na ulaghai kila mara kulalamika wakati ametupa akili za kufikiri vema na kutenda kwa tija. Mbowe na Lissu wakiwa watu waliopewa fikra nzuri na Mungu wameshindwa kuzitumia na CHADEMA imezama kwenye tope la volcano wakati CCM ikichanua kwa mipango.

Usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili taifa. Kumbe CHADEMA ingeshinda Mbowe na Lissu wangetuzamisha. Mungu ana makusudi yake na CCM itaendelea kutawala kwa matakwa ya Mungu wetu.
Tatizo ni ubinafsi. Mbowe na Lissu wanajali uchaguzi wa Rais na Wabunge tu kwa vile wao ndiyo wanaoshiriki. CC Erythrocyte
 
Iwe ni kweli kaongea BAGONZA au sio kweli. Ila Mbowe na Lissu wameiuwa CHADEMA. huwezi kushinda uchaguzi ambao hujajiandaa.
Unavuna ulichopanda
 
..Chadema iliuwawa na Magufuli akishirikiana na vyombo vya dola.

..chama kilikuwa kinaongeza idadi ya viongozi ktk kila uchaguzi mpaka pale Magufuli alipoamua kutumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema.
 
Wahariri wa jf mnafanya kazi bora sana.
Sasa ilepost ya kupotosha mbna bado inatrend?!
Ifuteni
 
Back
Top Bottom