SI KWELI Askofu Bagonza amesema CHADEMA imefifisha matumaini ya Watanzania

SI KWELI Askofu Bagonza amesema CHADEMA imefifisha matumaini ya Watanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Askofu Bagonza ni kiongozi maarufu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Zaidi ya kuwa kiongozi wa Dini Amekuwa akijihusisha sana na masuala ya kijamii na haki za binadamu nchini Tanzania. Mbali na majukumu yake ya kidini, Askofu Bagonza amekuwa akizungumzia mara kwa mara masuala ya kisiasa na kijamii, akisisitiza uwajibikaji, haki, na demokrasia.

Leo Oktoba 31, 2024 Mchungaji Peter Msigwa kupitia Akaunti yake ya Mtandao wa X amechapisha andiko lililoonekana kuwa ni la Jambo TV Tazama (hapa) lenye picha ya Askofu Bagonza pamoja na maneno CHADEMA IMEFIFISHA MATUMAINI YA WATANZANIA - ASKOFU BAGONZA

UPI UHALISIA WA TAARIFA HII?

JamiiCheck.com imefanya ufuatiliaji wa Mtandao na kubaini kuwa taarifa hiyo haijawahi kuchapishwa kwenye kurasa rasmi za Jambo TV kama linavyoonekana. Uchambuzi wetu umebaini kuwa Taarifa hiyo imezushwa na kufananishwa na machapisho ya Jambo TV ili kupotoshwa.

Aidha, Jambo TV kupitia kurasa zao rasmi wamejitokeza na kukanusha kuhusika na Taarifa hiyo. Katika kufafanua Jambo hilo wameandika:

Haya sio maudhui ya Jambotv_ , na hayako kwenye kurasa yoyote inayomilikiwa na JAMBO TELEVISION, sio sawa mtu wa kariba yako kushiriki hii michezo michafu inayoratibiwa na Chawa
1730394809380-png.3140017

Kanusho lililotolewa na Jambo TV​
Back
Top Bottom