Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
ASIYEUTAKA URAIS CCM HAJAZALIWA!
Wakristo tumo kwenye juma takatifu. Tunaalikwa kutohukumiana katika habari ya vyakula na vinywaji (Wakolosai 2: 16-17).
Ndani ya CCM tusihukumiane kwa habari ya kuutaka urais au kutoutaka. Urais ni sehemu ya CCM na CCM ni sehemu ya urais. Asiyeutaka urais CCM bado hajazaliwa:
1. Walio kimya wanautaka.
2 Wanaopiga kelele za kuonyana, wanautaka.
3. Wanaotamka hadharani kwamba hawautaki, hiyo ndiyo njia yao ya kuutaka.
4. Waliowahi kuutaka, hawajapona ugonjwa wa kuutaka.
5. Waliowahi kuwa nao, nao wanautaka. Kuuomba wanaona shida; lakini wakipewa watapokea kwa shangwe.
6. Waliopo wanautaka ndio maana wanao🤣
7. Wanaopata shida kuona wengine wanautaka, nao wanautaka na watamani hao wasiutake ili wao peke yao ndio wautake bila kutamka.
KWA HIYO: Mjadala wa urais ni wa CCM. Uondoeni hadharani. Upelekeni chumba chetu cha kulala tukavuane nguo huko huko. Watu wasubiri tuwaletee asiyeutaka kama tutampata!
Si kwamba Wajaluo hawana ndevu. Wanazo. Nyingine hazionekani hadharani na nyingine wananyoa. Kama Mungu alitaka tuwe na ndevu, asingeumba mkasi👍👍
Nawatakia Juma Takatifu lenye kuzingatia ukweli.