Askofu Bagonza atangaza ibada kurejea kuanzia Mei 31, waumini wote watatakiwa kuvaa barakoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Bagonza-620x308.jpg

Askofu Benson Kagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amesema, ibada zilizositishwa ili kujikinga na maambukizo ya ugonjwa unaotokana na virusi vya corona (COVID-19) zitarejea tarehe 31 Mei, 2020.

Tarehe 26 Aprili, 2020, Askofu Bagonza alitangaza kusitisha ibada na mikusanyiko yote akieleza sababu ya kufanya hivyo ni dayosisi hiyo kuwa mpakani na nchi ambazo raia wake wanatoroka na kuingia Tanzania.

Askofu Bagonza amesema, Ibada hizo zilisitishwa kwa kipindi cha wiki nne ili kuweka mazingira sawa.

“Tuliunda kikosi kazi kupitia maeneo mbalimbali na kazi imekamilika na tarehe 31 Mei, 2020 ibada zinarejea,” amesema Askofu Bagoza.

Akitaja baadhi ya mambo iliyobaini kikosi hicho iliyopitia makanisa yote 267 ya Dayosisi hiyo ni, “kila kanisa ziwepo Ibada mbili kila Jumapili na watu watapangwa kila kitongoji kuingia kanisani.”

Askofu Bagonza amesema, kila muumini atakayefika kanisani, atapaswa kuvaa barakoa ambapo tayari wamenunua barakoa zaidi ya laki moja.

“Tumenunua ‘themo scaner’ kupima joto, vitakasa mikono, ndoo na kila kanisa vifaa vitakuwepo bila shida,” amesema kiongozi huyo wa kiroho.

Amesema, kikosi hiko, kimebaini baadhi ya makanisa yana madirisha madogo, hivyo wamekubaliana kuyapanua pamoja na kufanya upuliziaji, “hata kama watalamu wamesema haiui, ila tunajihakikishia tunakuwa salama zaidi.”

Askofu Bagonza amesema, “makatazo mengine yamewekwa, ibada zinakuwa fupi na washirika wanakaa kwa kuzingatia umbali ili wasibanane. Haya yote tusingeweza kuyafanya wakati watu wakiwa ndani, ndiyo maana tuliamua kusitisha ili kufanya maboresho.”
 
That was a wrong move. Sasa kitu gani kilimfanya asimamishe huduma, na kitu gani kimebadilika hadi kuamua kuendelea?

Lockdown is a short term strategy. Huwezi pambana na corona kwa kuweka watu lock down. Mwishoni mwa siku, lockdown itaondolewa nchi zote, ingawa corona bado itakuwepo
 
Bagonza-620x308.jpg

Askofu Benson Kagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amesema, ibada zilizositishwa ili kujikinga na maambukizo ya ugonjwa unaotokana na virusi vya corona (COVID-19) zitarejea tarehe 31 Mei, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 26 Aprili, 2020, Askofu Bagonza alitangaza kusitisha ibada na mikusanyiko yote akieleza sababu ya kufanya hivyo ni dayosisi hiyo kuwa mpakani na nchi ambazo raia wake wanatoroka na kuingia Tanzania.

“Tuliunda kikosi kazi kupitia maeneo mbalimbali na kazi imekamilika na tarehe 31 Mei, 2020 ibada zinarejea,” amesema Askofu Bagoza.

Akitaja baadhi ya mambo iliyobaini kikosi hicho iliyopitia makanisa yote 267 ya Dayosisi hiyo ni, “kila kanisa ziwepo Ibada mbili kila Jumapili na watu watapangwa kila kitongoji kuingia kanisani.”

Askofu Bagonza amesema, kila muumini atakayefika kanisani, atapaswa kuvaa barakoa ambapo tayari wamenunua barakoa zaidi ya laki moja.
“Tumenunua ‘themo scaner’ kupima joto, vitakasa mikono, ndoo na kila kanisa vifaa vitakuwepo bila shida,” amesema kiongozi huyo wa kiroho.

Amesema, kikosi hiko, kimebaini baadhi ya makanisa yana madirisha madogo, hivyo wamekubaliana kuyapanua pamoja na kufanya upuliziaji, “hata kama watalamu wamesema haiui, ila tunajihakikishia tunakuwa salama zaidi.”

Askofu Bagonza amesema, “makatazo mengine yamewekwa, ibada zinakuwa fupi na washirika wanakaa kwa kuzingatia umbali ili wasibanane. Haya yote tusingeweza kuyafanya wakati watu wakiwa ndani, ndiyo maana tuliamua kusitisha ili kufanya maboresho.”
KKKT Chadema.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Back
Top Bottom