Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Asante baba Askofu, hii nchi ilipofika viongozi na watawala wanauwezo wa kutenda maovu zaidi kuliko kutenda Mema.
 
Bagonza tunajua ni kaada wa Chadema


Km Kweli anakipenda chama chake asimuogope Mbowe amwambie arudishe bilion 8

Ni kama hukusoma na kuelewa bandiko la askofu. Amesema rushwa haina chama wala dini. Anashauri hata tuwe na mfumo badala ya uthubutu!

Swala lako dhidi ya Mbowe halikupaswa kuwa katika sentinsi moja na CHADEMA! Uchunguzi dhidi ya Mbowe uendelee kama ambavyo uendelee dhidi ya Chenge, Tibaijuka na wengine bila kuangalia vyama wala dini zao. Je hilo ndio linaendelea??
 
Bagonza na wenzake wajikite zaidi kuzungumzia mambo yanayoendana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao za dini na si vinginevyo.,
Jiulize mwenyewe kama post yako ni ya kiwango. Je, kwa elimu uliyonayo unastahili kuandika hivi ulivyoandika?
 
Kuwahi kuchangia kila thread ilihali hata maudhui yake hujaelewa haina tofauti na kahaba anaye anza kukata mauno baada ya kuona pochi nene kumbe hata nguo ya ndani (pichu) hajaivuwa.
Hiyo ndio tabia yako uliyo bobea
 
Sikatai ila mahaba ya Askofu boganza kwa Chadema yanafanya aogope hata kumkosoa Mbowe

Tunaambiwa Askofu boganza ni mshauri wa Chadema ila Kwanini anaogopa kumkosoa Mbowe
Ya kuambiwa changanya na yako
 

Huyu mchunga Kondoo wa Mungu si ndiye aliyezushiwa kesi ya Uraia au kuna mwingine?
Yuko vizuri na ana hoja za msingi sana katika hili la RUSHWA hasa TAKUKURU vs CAG!
Mtu atajiuliza hivi:
  1. TAKUKURU WALIKUWA/WANAKUWA WAPI WAKTI WATU WANATAFUNA MAMILIONI/MABILIONI YA WALIPA KODI?
  2. TAKUKURU WALIKUWA/WANAKUWA WAPI WATU WANAPOPEANA NGONO KAMA RUSHWA?
  3. JE, TAKUKURU NI KITENGO CHA KUMSAIDIA CAG KUFUATILIA WIZI, RUSHWA NS UBADHIRIFU?
  4. JE, NANI ANAINGILIA MAMLAKA YA MWENZIE HAPA?
Maswali ni mengi yanayokosa Majibu mujarabu!!!
 
Kwanini inatumika nguvu kubwa ya kupinga takukuru wasifanye kazi Yao? Kuna nini chadema mpaka wanaogopa?
Mkuu kinachowashangaza watu wengi ni kuona takukuru haijaanzia uchunguzi huko ccm,tena huko ccm hawali michango ya wanachama wao waliojiunga huko kwa hiari yao bali wanaiba hata pesa za umma.Sometimes natamani kuwa gaidi
 
Imeelezwa kuwa TAKUKURU wamejipa/wamepewa kazi ya kuchunguza namna michango ya wabunge wa cdm ilivyotumika.
Mungu halali. Je, michango mbalimbali wanayotoa wananchi kwa vyama vingine vya siasa mabilioni kwa mabilioni nayo inakaguliwa na TAKUKURU? Uchunguzi huo wa TAKUKURU unatokana na hofu tu. CDM
 
Tatizo lako " you do not read between lines" . Umemwelewa Baba Askofu anachosema? Rudia kusoma uzi tena au huna mda? Hongera!
 
Sio huyu ila wapo maeneo ya karibu huyu akiongoza kkkt yule mwingine ni Katoliki.
 
Tatizo lako " you do not read between lines" . Umemwelewa Baba Askofu anachosema? Rudia kusoma uzi tena au huna mda? Hongera!
Huyo huwa anaishia soma heading chakubanga anamlipa hapa jukwaani kwa ajili ya kupinga yachomayo ccm na serikali usiwe unasumbuka kum'quote ni sawa na kumfundisha mbuzi kudansi hatakukuelewa.
 
Huyu askofu very smart daaa
 
Mkuu unaijua elimu yangu ni kiwango gani?
Ndiyo maana nikasema jiulize kwa kiwango ulicho nacho cha elimu. Hivi kweli unastahili kuandika ulivyoandika?. Kama shule yako ni kiwango cha Dr. Bagonza, basi nihitimishe kuwa huitendei haki elimu yako kwa sababu ya uono hafifu ulionao. Maana utakuwa ni msomi anayeishi kishabiki. Kibaya zaidi kama ukiwa kiongozi wa Taasisi basi taasisi hiyo itakuwa ni moja ya weak institution, kama zilivyoainishwa na Acemoglu and Robinson katika kitabu chao "WHY NATIONS FAIL". Unatia aibu taaluma kwa kumshambulia mtu badala ya hoja iliyoko mezani.
 
Si unaona santuri za RC wa Mbeya na Dar. Akianzisha wa Dar yule wa Mbeya anadakia chapchap kukoleza wimbo wa kwaya aipendayo Jiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…