amtoni mwaihesya
Member
- May 31, 2019
- 86
- 86
Sheria za ukaguzi kama nakumbuka vizuri zinasema "Taarifa ya Mkaguzi Mkuu kwa Hesabu zilizokaguliwa, hazipaswi kuhojiwa na MTU yeyote" sasa hii imekaje? Tusaidieni NAO
Bila shaka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bila shaka
Bagonza tunajua ni kaada wa Chadema
Km Kweli anakipenda chama chake asimuogope Mbowe amwambie arudishe bilion 8
Huyu mzee ishu ya uraia inamnyima usongizi .bangoza ni mganda pure
Jiulize mwenyewe kama post yako ni ya kiwango. Je, kwa elimu uliyonayo unastahili kuandika hivi ulivyoandika?Bagonza na wenzake wajikite zaidi kuzungumzia mambo yanayoendana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao za dini na si vinginevyo.,
Kuwahi kuchangia kila thread ilihali hata maudhui yake hujaelewa haina tofauti na kahaba anaye anza kukata mauno baada ya kuona pochi nene kumbe hata nguo ya ndani (pichu) hajaivuwa.CAG huwa anakagua vitu vichache
Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe
Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua
Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
Mkuu unaijua elimu yangu ni kiwango gani?Jiulize mwenyewe kama post yako ni ya kiwango. Je, kwa elimu uliyonayo unastahili kuandika hivi ulivyoandika?
Ya kuambiwa changanya na yakoSikatai ila mahaba ya Askofu boganza kwa Chadema yanafanya aogope hata kumkosoa Mbowe
Tunaambiwa Askofu boganza ni mshauri wa Chadema ila Kwanini anaogopa kumkosoa Mbowe
"Ni halali mtu kujiuliza TAKUKURU wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri- KKKT Dayosisi ya Karagwe
Htr sn hii injihao sasa hivi wanacheza na hisia za mkulu ili mkono uende kinywani. wanaogopa wakiwa kinyume watatumbuliwa. ni mwendo wa kufanya kazi kinafiki zaidi.
Shithole countryKweli
Mkuu kinachowashangaza watu wengi ni kuona takukuru haijaanzia uchunguzi huko ccm,tena huko ccm hawali michango ya wanachama wao waliojiunga huko kwa hiari yao bali wanaiba hata pesa za umma.Sometimes natamani kuwa gaidiKwanini inatumika nguvu kubwa ya kupinga takukuru wasifanye kazi Yao? Kuna nini chadema mpaka wanaogopa?
Imeelezwa kuwa TAKUKURU wamejipa/wamepewa kazi ya kuchunguza namna michango ya wabunge wa cdm ilivyotumika.CAG huwa anakagua vitu vichache
Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe
Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua
Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
Tatizo lako " you do not read between lines" . Umemwelewa Baba Askofu anachosema? Rudia kusoma uzi tena au huna mda? Hongera!CAG huwa anakagua vitu vichache
Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe
Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua
Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
Sio huyu ila wapo maeneo ya karibu huyu akiongoza kkkt yule mwingine ni Katoliki.Huyu mchunga Kondoo wa Mungu si ndiye aliyezushiwa kesi ya Uraia au kuna mwingine?
Yuko vizuri na ana hoja za msingi sana katika hili la RUSHWA hasa TAKUKURU vs CAG!
Mtu atajiuliza hivi:
Maswali ni mengi yanayokosa Majibu mujarabu!!!
- TAKUKURU WALIKUWA/WANAKUWA WAPI WAKTI WATU WANATAFUNA MAMILIONI/MABILIONI YA WALIPA KODI?
- TAKUKURU WALIKUWA/WANAKUWA WAPI WATU WANAPOPEANA NGONO KAMA RUSHWA?
- JE, TAKUKURU NI KITENGO CHA KUMSAIDIA CAG KUFUATILIA WIZI, RUSHWA NS UBADHIRIFU?
- JE, NANI ANAINGILIA MAMLAKA YA MWENZIE HAPA?
Huyo huwa anaishia soma heading chakubanga anamlipa hapa jukwaani kwa ajili ya kupinga yachomayo ccm na serikali usiwe unasumbuka kum'quote ni sawa na kumfundisha mbuzi kudansi hatakukuelewa.Tatizo lako " you do not read between lines" . Umemwelewa Baba Askofu anachosema? Rudia kusoma uzi tena au huna mda? Hongera!
CAG na TAKUKURU
Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.
Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:
1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti![emoji23] Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.
2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:
1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.
2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?
3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.
Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.
Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
Jiwe naye arudishe 1.5TrilioniBagonza tunajua ni kaada wa Chadema
Km Kweli anakipenda chama chake asimuogope Mbowe amwambie arudishe bilion 8
Ndiyo maana nikasema jiulize kwa kiwango ulicho nacho cha elimu. Hivi kweli unastahili kuandika ulivyoandika?. Kama shule yako ni kiwango cha Dr. Bagonza, basi nihitimishe kuwa huitendei haki elimu yako kwa sababu ya uono hafifu ulionao. Maana utakuwa ni msomi anayeishi kishabiki. Kibaya zaidi kama ukiwa kiongozi wa Taasisi basi taasisi hiyo itakuwa ni moja ya weak institution, kama zilivyoainishwa na Acemoglu and Robinson katika kitabu chao "WHY NATIONS FAIL". Unatia aibu taaluma kwa kumshambulia mtu badala ya hoja iliyoko mezani.Mkuu unaijua elimu yangu ni kiwango gani?
Si unaona santuri za RC wa Mbeya na Dar. Akianzisha wa Dar yule wa Mbeya anadakia chapchap kukoleza wimbo wa kwaya aipendayo Jiwe."Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
mkuu Pascal Mayalla naomba kwa heshima naomba hii point ianzishie uzi ktk zile nyuzi zako za maslahi mapana ya taifa