Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.

Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:

1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti!😂 Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.

2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:

1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.

2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?

3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.

Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.

Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
 
"Ni halali mtu kujiuliza TAKUKURU wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri- KKKT Dayosisi ya Karagwe
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
 
"TAKUKURU wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti!" Dk. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Dayosisi ya Karagwe
 
"Ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa. Watu wote, taasisi zote za umma na binafsi, rushwa inaweza kufanyika ndani yake" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Dayosisi ya Karagwe
 
Yaani takukuru wanaacha kumchunguza rais anayefanya manunuzi mbalimbali yakiwemo ya ndege kwa siri tena bila kufuata sheria ya manunuzi wanahangaika na chadema?
Yaani badala kufanya uchunguzi zilipo trilioni 1.5 zilizoibuliwa ma cag wanahangaika na beat za kisiasa? WHY? KWA NN?
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua TAKUKURU. Kinadharia pia, TAKUKURU wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Karagwe
 
"Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili (CAG&TAKUKURU), siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Dayosisi ya Karagwe https
 
"Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
mkuu Pascal Mayalla naomba kwa heshima naomba hii point ianzishie uzi ktk zile nyuzi zako za maslahi mapana ya taifa
 
Sikatai ila mahaba ya Askofu boganza kwa Chadema yanafanya aogope hata kumkosoa Mbowe

Tunaambiwa Askofu boganza ni mshauri wa Chadema ila Kwanini anaogopa kumkosoa Mbowe
Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua TAKUKURU. Kinadharia pia, TAKUKURU wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Karagwe
 
Bagonza tunajua ni kaada wa Chadema


Km Kweli anakipenda chama chake asimuogope Mbowe amwambie arudishe bilion 8
"Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu" Askofu Dkt. Benson Bagonza
 
Yaani takukuru wanaacha kumchunguza rais anayefanya manunuzi mbalimbali yakiwemo ya ndege kwa siri tena bila kufuata sheria ya manunuzi wanahangaika na chadema?
Yaani badala kufanya uchunguzi zilipo trilioni 1.5 zilizoibuliwa ma cag wanahangaika na beat za kisiasa? WHY? KWA NN?
hao sasa hivi wanacheza na hisia za mkulu ili mkono uende kinywani. wanaogopa wakiwa kinyume watatumbuliwa. ni mwendo wa kufanya kazi kinafiki zaidi.
 
"Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo" Dkt. Benson Bagonza
Pitia hizi hints huyu mzee ni kichwa hasa cc neo1
 
Bia yetu inakuhusu hii
"Tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
 
Bia yetu inakuhusu hii
"Tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
 
"Ni halali mtu kujiuliza TAKUKURU wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri- KKKT Dayosisi ya Karagwe
yule Pasto fake wa River side ubungo ataisoma hii?
 
Back
Top Bottom