Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Huyu Askofu Bagonza na Niwermugizi Ni mabaki ya Lowasa yaliyobaki chadema Hawa hawakuwa wanasiasa kabla ila Lowasa alipoanza harakati zake Ni katika waliopewa maburungutu ya pesa za Lowasa wikuwa viongozi wengi wa dini waliolamba pesa za Lowasa wakaona siasa so ndio hii !!! Wakaacha madhabahu wakawa wanaimba pambo za Mabadiliko Lowasa,Lowasa mabadiliko!!! Badala ya kuimba pambio za Mungu

Wenzao wengi wameachana na Siasa na kurudi madhabahuni Hawa wawili Askofu Niwermugizi na Bagonza Bado wanaota hela za wanasiasa wa Chadema wakingoja kwa Subira kuwa iko siku zitakuja Tena kupitia chadema badala ya kumsubitia Yesu kuwa atakuja Tena duniani kuwachukua wateule wake
Ni dhana za kitoto
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
Hupitwi$
 
...
3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.
....
"Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ..." What a statement! Barikiwa sana Baba Askofu.
 
Kwangu mimi Bagonza ni muhuni tu!
Kwa akili yake anafikiri Mbowe ni malaika asiyeweza kukosea? Hii tabia ya kumkingia mtu kifua kisa una maslahi nae kina Bogonza wapo nayo hadi makanisani huko wanakoongoza.
Muumini mwenye hela akikosea huwezi kumkuta Bagonza akimkanya kwa kuwa ana maslahi nae tofauti na maskini!

Bagonza yeye anafuatilia zaidi siasa kuliko kazi yake aliyonayo!

Kiki yake ya kufunga kanisa imemtokea puani ana hasira sana.
 
Huyu Askofu aguswe aandike kitabu.. Ntakuwa wa kwanza kununua..
Ana falsafa nyingi saana
Ni hatari saana mtu kama huyu kuondoka bila kuacha maandishi kwenye kitabu
Hana lolote tabia yake ni unafiki!
Mtu mnafiki kamwe hawezi kuwa mtu wa maana
 
Ubovu Wa takukuru unaanzia pale wanapofanya kitu kwa maagizo.Mbaya zaidi wanatumwa Na wanasiasa...
 
Bagonza yeye anafuatilia zaidi siasa kuliko kazi yake aliyonayo!

Kiki yake ya kufunga kanisa imemtokea puani ana hasira sana.

Askofu Bagonza kama raia mwingine ana uhuru wa kutoa mawazo yake kwa faida ya nchi yake. Sio kila mtu anaekosoa serikali ni mfuasi wa Chadema! Kama unamfuatilia maoni yake ni ya busara na hekima sana.

Nakushangaa sana unaposema kiki yake ya kufunga kanisa imemtokea puani kwa lipi? Kwa kufunga kanisa Askofu alionesha uongozi na ubinadamu wa hali ya juu wa kujali maisha ya waumini wake. Naamini kabisa katika nchi tusiyopima waathirika wa corona, Baba askofu Bakonza amefanya kazi ya kimungu kulinda afya za kondoo anaowaongoza.
 
Hana lolote tabia yake ni unafiki!
Mtu mnafiki kamwe hawezi kuwa mtu wa maana

Acha kubwabwaja toa ushahidi wa unafiki wake. Huyu Baba Askofu ni mtu mwenye hekima ,shujaa na ana busara pia; sio kama ninyi mkishindwa kwa hoja mnaanza kuwaita watu majina eti ooh huyu ni kada wa Chadema. Jibuni hoja kwa hoja!!!
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?
CAG huwa inafuatilia taratibu nzima za malipo. Nani kaanzisha, nani kaidhinisha na uhalali wa malipo hayo. Hatoridhika kuambiwa tu kuwa pesa hii nililipa deni la chama.

Atataka kuona minutes za kikao kilichoidhinisha kukopa na kwa nini walikopa. Watataka kuona makubaliano ya mkopo huo. Kama ni mkopo wa fedha, atataka kuona ushahidi wa kama kweli pesa hizo ziliingia.

Kama ni vifaa, ushahidi wa nani alivipokea kwa maandishi n.k. Atafuatilia namna mkopo huo ulivyotumika. Kama wanamlipa aliyewakopesha, watataka kuona analipwa vipi, akaunti inayolipiwa n.k. Si rahisi kumdanganya na kumficha matumizi yaliyotumika nje ya taratibu.

Hasa katika Chama Kikuu cha upinzani. Nadhani tofauti yake na TAKUKURU ni kuwa CAG haangalii hisia au makusudio, yeye anajikita kwenye uhalisia.

Amandla...
 
Sikatai ila mahaba ya Askofu boganza kwa Chadema yanafanya aogope hata kumkosoa Mbowe

Tunaambiwa Askofu boganza ni mshauri wa Chadema ila Kwanini anaogopa kumkosoa Mbowe

Bia yetu sante sana kwa mchango wako . nisaidie swala moja . wewe unaujasiri wa kumkosoa mwenyekiti wako wa CCM Taifa?
 
*KUTOKA KWA BABA ASKOFU DR BENSON KALIKAWE LWAKALINDA BAGONZA KUHUSU TAKUKURU NA CDM*
-----------------------------------
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.

Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:

1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti![emoji23] Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.

2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:

1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.

2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?

3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.

Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.

Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
 
Back
Top Bottom