The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
VILIVYOUMBWA HAVINA U-milele!
Nimetoka kanisani. Watu walifunga ndoa nyingi jana. Leo wamekuja wachache. Nimekuta Gen Z Masalia wamejaza simu yangu kwa maswali yaliyoibuliwa na Gen Z mwenzao anayedai kuna chama kitaishi milele au mpaka mwisho wa dunia. Wanataka kujua nina maoni gani? Nasema hivi:
1. Sitakuwepo mwisho wa dunia ili kuona kama chama hicho kitakuwepo.
2. Hata yeye hatakuwepo kutukumbusha kuwa mwisho wa dunia umefika na chama bado kipo.
3. Chama hufa kikianza kufikiri hakitakufa. Kama kimeanza. Wanachama waandae rambirambi.
4. TAA ilikufa, ikazaliwa TANU. Na TANU ikafa, ikazaliwa CCM. Hii nayo imeanza kufikiri haitakufa?!. Fikra hizo ni tangazo la tuandae rambirambi.
5.Hakuna U-milele katika vitu vilivyoumbwa au kuundwa. Muumbaji hudumu milele. Muundaji hufa. Hakuna muasisi wa chama hicho aliye hai. Lakini muumbaji yupo. Ndiye aliumba mwisho wa dunia. Mwisho wa dunia utapita, na yeye atabaki.
Nimemwangalia kijana huyo. Macho yake yanasema tofauti na mdomo wake. Ndiyo maana mashahidi hawatakiwi kufichwa. Macho yakiandamana na midomo ikarusha mabomu tunapata ukweli. Yeye ni rafiki yangu. Anapenda uchochezi kwa sababu ya kinga🤣. Ni kawaida ya vijana kutamani umilele. Wanaruhusiwa kufanya makosa. Hamuoni kuwa anafanana na Wajaluo?
Hakuna atakayebaki ni Gen Z. Kuna siku mtakuwa kama mimi na mtani wangu Wasira.
Jumapili Njema