PostGE2025 Askofu Bagonza: Desemba 9 ni siku ya Uhuru wetu, siyo siku ya Miundombinu tu

PostGE2025 Askofu Bagonza: Desemba 9 ni siku ya Uhuru wetu, siyo siku ya Miundombinu tu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Anaandika Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasa wake wa Facebook;

"Kuahirisha maadhimisho ya Uhuru na fedha kutumika kukarabati Miundombinu. Hii pia ni nzuri. Mtoto wa Mjaluo akinya, mzazi ndio huzoa kinyesi cha mtoto. Na mtoto wa Mkurya akinyea mbeleko, anabebwa humo humo! Ni bora mtoto anye kuliko kuwa na mtoto asiyeenda choo kabisa. Nishauri matatu:

a) Familia zimefiwa, zina majeruhi, zina hasara ya mali nk. Najiaminisha kwamba kukarabati miundo mbinu ni mwanzo, wala si mwisho.

b) Desemba 9 ni siku ya Uhuru wetu, siyo siku ya Miundombinu tu. Msiba tuliomo utukumbushe thamani ya uhuru wetu. Viongozi wajikite kuulinda na kuuongeza, si kuupunguza. Uhuru wa watu umepunguzwa MNO. Uhuru wa nchi ni uhuru wa wananchi, si wa viongozi tu.

c) Tusipuuze tishio la Desemba 9. Tukipuuza, hatutamaliza ukarabati. Tupate ujasiri na hekima kukabiliana na changamoto hii. Tuache kuandaa risasi na mabomu. Tuandae haki, hekima, ustahimilivu, ukweli, na unyenyekevu usio udhaifu. Tuongeze kujilaumu kuliko kulaumu wengine. Tuitumie hazina ndogo ya UWAJIBIKAJI iliyobaki Stoo.

NINAAMINI, kuwajibika ni heshima kuliko kuwajibishwa. Serikali yetu siyo dhaifu lakini imejeruhiwa sana na mapema sana. Tuendako ni mbali bila umoja na mshikamano."
 
Back
Top Bottom