Askofu Bagonza: Jaji Mwangesi Pokea Mzigo toka kwa CAG

Jaji Mwangesi Pokea Mzigo toka kwa CAG

Kila mfumo una uwezo wa kujiharibu. Demokrasia ina uwezo wa kujiua. Udikteta una uwezo wa kujiua ndani yake. Uliberali unayo sumu yake. Si sumu ya kuua mifumo mingine bali kujiua. Tumeona jinsi awamu ya tano ilivyotengeneza sumu ya kujiua. Ilipobana Uhuru wa maoni, Uhuru wa vyombo vya habari, Uhuru wa bunge, Uhuru wa vyama vya siasa, Uhuru wa mahakama na mawakili na Uhuru wa kiuchumi, ilikuwa imetengeneza sumu ya kujiua. Sumu hiyo inaitwa WASIOJULIKANA na ilikuwa inauzwa duka moja tu: IKULU.

Ameingia mpangaji mpya, duka limefungwa. Ameleta Odita (Auditor). Anaitwa CAG. Amekagua akakuta madudu. Giza lilipoingia, wadudu walikula kila kitu mpaka wakala moyo wa mpangaji aliyekuwemo. Ahsante CAG.

Jaji Mwangesi, Kamishna wa Maadili ana kazi ya kufanya. Apokee mzigo toka kwa CAG. Hawa wadudu waliokula bila kunawa wakaguliwe mali zao. Ndege haikutengenezwa lakini yawezekana ilijengwa hoteli binafsi mahali fulani. Fedha zilipopita Zimamoto zilienda wapi? Kuna watu ni matajiri kuliko vitengo walivyoviongoza. Ifanyike Audit ya wahusika. Mtu alikuwa Lodi Lofa jumapili, kesho yake ni tajiri wa Kikurya au Kizanaki😂😂 .

Nirudie tena: Nyumba yetu ya kupanga iliyo Magogoni na Chamwino inahitaji mkataba mpya wa wapangaji. Si kila mpangaji anayeingia aje na yake. Kuna wengine wanapaka kinyesi kuta zetu. KATBA MPYA, MKATABA MPYA. Asiyependa abaki na kodi yake. Tukikosa wapangaji tutafugia kuku, nguruwe ni haramu.
Mzigo toka kwa CAG

wasiojulikana wameingia hadi kwenye fedha wameweka mil 200 na za zimamoto na kuziondoa bila kujulikana
 
Kutoka awamu ya tano nimejifunza Kuwa ubebe si kitu kizuri. Kwa hiyo, kwa vile mimi ni baba na mahalipengine ni boss, naahidi kuacha kabisa ubabe kwa wale walio chini yangu.
 
mungu ametuumba tuttende yaliyo mema hatukkuumbwa tutende mabaaya hiyo ni kazii ya shetani na maapepo yyake
 
.
20210407_163341.jpg

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Awamu ya mwendazake imekuja na funzo,kuwatambua wachungaji,maaskofu na mashehe wa kweli na wachumia tumbo.heshima sana kwenu Bagonza ,Mwamakula na wengineo mliosimamia mlichokiamini mpaka dakika ya mwisho licha ya vitisho na misuko suko mliyokutana nayo.
Ameeen
 
Back
Top Bottom