Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
Kumekuwa na memo maarufu kuwa vijana
"wameshawishiwa" na watu waishio nje ya nchi. Yani watawala wanakiri kwamba vijana hawajalazimishwa, kuburuzwa, kutishwa wala kuhongwa. Bali wameshawishiwa kwa hoja. Nami nashawishika kuwashawishi watawala wetu watumie ushawishi ili kuongea na vijana kwa sababu zifuatazo;
1. Kuandamana ni haki ya kikatiba. Serikali isitutumie nguvu kuvunja katiba. Itumie ushawishi. Tuwashawishi vijana
waahirishe haki yao ya kikatiba na siyo kuwatisha.
2. Kabla ya Oktoba 29, tulitumia vitisho kuzuia maandamano.
Vitisho havikusaidia. Mganga aliyetudanganya kuwa vitisho vinafaa yeye ndiye hafai. Tusiendelee kumuamini.
3. Mawaziri na viongozi wametawanyika nchi nzima kuongea
na makundi mbalimbali na kujaribu kuyashawishi. Polisi na watawala mnaotumia lugha za kibabe mnawavunja moyo.
4. Kabla ya Oktoba 29, tuliimba sana wimbo wa AMANI na hatukutaka kabisa kusikia wimbo wa HAKI. Bahati mbaya wimbo wa AMANI haukupendwa na haukulipa. Wanaoendelea kuimba wimbo huo wanapoteza muda na kuchochea hasira.
Matunda ya wimbo huo tumeyaona. Sasa waimbieni wananchi wimbo wa HAKI japo kuwapa matumaini.
5. Tulitia sahihi mkataba wa haki za watoto. Haki yao moja kubwa ni KUSIKILIZWA. Matokeo ya mkataba huo ni kuwa wazazi, walimu, polisi, mahekalu na serikali zote zinaogopa watoto. Watoto WANAOGOPWA lakini HAWAOGOPI.
Wakikuhurumia watakunywa sumu kuliko kufuata UBABE
wako. Mlio wazazi mnajua nisemacho. Kama wamekushinda watoto wa nyumbani kwako, utawaweza wa mtaani?
Kwa mara nyingine nawashauri, PUNGUZENI UBABE, ONGEZENI USHAWISHI (Serikali inayokiri kuzidiwa ushawishi na watu wachache walio nje ya nchi, impoteza sifa ya kuwa serikali.