The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Askofu Benson Bagonza kupitia ukurasa wake wa Facebook anasema;
UDINI UNAWEZA KUWA HUU.
Suala la udini katika taifa letu ni mgumu kuuthibitisha. Unachoweza ni kuonyesha au kuona dalili. Ukiona hali hiyo, wewe binafsi unachukua hatua;
1. Kumbagua mtu kwa sababu ya dini yake ni UDINI.
2. Kufikiri unakataliwa au unakubaliwa kwa sababu ya dini yako ni UDINI.
3. Kuteua au kuagiza kigezo cha dini kuwa moja ya vigezo vya kutafuta watakaoteuliwa ni UDINI.
4. Kuona kwa kuhesabu kuwa dini yako imepunjwa katika uteuzi ni UDINI.
5. Kuona kwa kuhesabu na kufurahi kuwa dini yako imepata haki katika uteuzi ni UDINI.
6. Kutumia historia na kusema dini yako ilionewa na sasa imejitambua ni UDINI.
7. Kutumia historia na kusema nafasi fulani haijawahi kushikiliwa na dini yangu ni UDINI.
8. Kutumia takwimu ili kudai dini yako ipewe haki fulani ni UDINI.
9. Kumkosoa au kumpinga kiongozi fulani kwa kuwa ni wa dini fulani ni UDINI.
10. Kumuunga mkono au kumtetea kiongozi fulani kwa kuangalia dini yake ni UDINI.
11. Kujifanya huoni udini katika hali tuliyo nayo ni UDINI.
12. Kuwanyima uteuzi watu fulani kwa sababu ya dini zao au kwa sababu ya ukaribu wao na viongozi wa dini fulani ni UDINI.
13. Kuikana dini yako au kubadili mwonekano wako huonekane ni wa dini fulani wakati si wa dini hiyo, ni UDINI.
14. Kunifikiria mimi mdini kwa kuwa ninachambua udini, ni UDINI.
15. Kuita watu walio tofauti nawe kiimani kuwa ni Makafiri ni UDINI.
16. Kujiona wewe si Kafiri wakati unabishana na Makafiri ni UDINI.
17. Kumkamata anayesema “Tutatoka” na kumchekea anayesema “tutakata viuno vyote” ni UDINI.
18. Kuitetea serikali kuliko inavyojitetea ni UDINI. Kinachofuata ni kuiharibia kuliko inavyojiharibia.
Orodha inaendelea…
Na KAFIRI MFAWIDHI MWANDAMIZI.