Askofu Bagonza: Maadili ya madaraka wakati wa vita

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
MAADILI YA MADARAKA WAKATI WA VITA

Taifa letu liko vitani. Tunapambana na adui asiyeonekana kwa macho bali kwa mashine kali ya kisasa iliyo DsM. Tunachokiona kwa macho ni majeruhi, vifo, mazishi na majonzi.

Mara tuone askari yule kavunjika mguu, mara yule kanyofolewa macho yote na kamanda yule wa kikosi kapotelea msituni haonekani tena. Kwa hiyo, hatuwezi kaa chini tukalia tu na hatuwezi kulialia bila utaratibu. Ndiyo maana, wakati wa vita mbaya, shughuli nyingine husimama na wote huingia vitani. Mnaoshangaa habari ya mazishi, mkumbuke vita ambayo makaburi huchimbwa mapema hata kabla watu hawajafa ili kuokoa muda pale watakapokufa!

Inapotokea kamanda kafia vitani, sharti mwingine aingie nafasi yake. Likitokea hilo, tuwe wavumilivu kwa sababu:

1. Wapo watakaomtazama anayeteua

2. Wapo watakaomtazama aliyeteuliwa

3. Wapo watakaomtazama aliyeondoka.

4. Wapo watakaoitazama nchi.

Yote haya hayakai kwa amani katika kikapu kimoja. Ndio maana diplomasia, mawasiliano ya umma na uratibishaji ni muhimu kiliko uteuzi wenyewe. Likikosekana moja kati ya hayo, vita-mama na adui husimama na vita mpya ya kupambana na maoni huanza. Tusiwachukie wanaojadili wakati mjadala tumeuanzisha sisi.

Tarehe 22 Novemba 1963, Rais JF Kenedy wa Marekani aliuawa huko Dallas, Texas Marekani. Masaa machache baadaye siku hiyo, Makamu wake Lyndon Johnson aliapishwa kwa dharura akiwa kwenye ndege (si Ikulu) katika uwanja wa Dallas. Aliitwa jaji mmoja wa mahakama toka hapo Dallas akapanda ndani ya ndege (Air Force One), kiapo kikachukuliwa. Taifa lilikuwa katika taharuki na ulazima wa kumrithi mkuu wa nchi ulipewa nafasi kwa mujibu wa katiba yao (Running mate system).

Vita tuliyo nayo kama nchi kwa sasa ni tofauti. Kwa maoni yangu, tuna matatizo makubwa mawili:

1. Tunapigana vita nyingi kwa wakati mmoja. Tunapigana na Covid 19, tunapigana na mabeberu, tunapigana na uhuru wa maoni, tunapigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya kundi moja na tunapigana na maaskari walio msitari wa mbele (watoa huduma).

2. Tunalazimisha upya wa kila kitu. Kuna mambo katika medani za kivita hayabadiliki hata kama kauli mbiu yetu ni kuleta UPYA wa kila kitu. Mathalani, waitwao wasaidizi na washauri sharti wawe huru, weredi na uwezo kuliko wanayemshauri, vinginevyo hawana sababu ya kuwepo. Gari tani 10 limekwama, huwezi peleka lori tani 3 kulikwamua! Tuwaheshimu wasaidizi na wataalam wakati wa vita.

Kumradhi, hata mimi kwa maoni haya nimeongeza idadi ya vita katikati ya vita zinazoendelea! Ndugu msomaji wa ukurasa wangu, yakikukera ziite kelele cha chura zisizoweza kumzuia mchota maji. Tuchape kazi.

Source page yake
FB_IMG_1588499091592.jpg
FB_IMG_1588499101189.jpg

View attachment 1438555View attachment 1438556

Source page yake
Duh umetuongezea Vita ya sita baba askofu😭😭😭😭😭😭
 
Umenikumbusha kisa cha kuhani Kayafa na mtawala Herode.
Ushirika uliolazimika kwa sababu ya uadilifu wa Bwana Yesu kwa ule wito alioujia duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom