PostGE2025 Askofu Bagonza: Mazingira ya sasa hayaruhusu maridhiano ya kweli bila uwajibikaji

PostGE2025 Askofu Bagonza: Mazingira ya sasa hayaruhusu maridhiano ya kweli bila uwajibikaji

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza, amesema mazingira ya sasa nchini hayaruhusu mazungumzo ya maridhiano kufanyika moja kwa moja kwa sababu bado hakuna uaminifu wa kutosha, mfumo wa kuaminika, wala dhamira ya wazi ya kukiri makosa. Amesema jamii imejengewa imani kwamba kila mtu ana bei na kwamba serikali haijawahi kushindwa, jambo linalozuia maridhiano ya kweli.

bagonza-px.jpg
Katika andiko lake katika ukurasa wake wa Facebook, Askofu Bagonza amesema maridhiano ya kidugu hayahitaji kuanza kwenye meza ya majadiliano, bali yafanyike kwanza kwa vitendo. Anashauri kusitishwa mara moja kwa vitendo vya utekaji, ukamataji kiholela na mateso ambayo amedai yanaendelea kuchochea hofu na mpasuko. Ameitaka serikali kuwaachia bila masharti wale wote waliotekwa, kuwekwa mahabusu au kufunguliwa mashitaka ya kisiasa.

Askofu amesisitiza umuhimu wa familia kupewa miili ya wapendwa wao bila kufichwa, ili waweze kuaga, kuomboleza na kumaliza msiba wao kwa heshima. Ameonya kwamba ni hatari taifa kuwa na watu wanaokimbia nchi kwa sababu ya misimamo yao, na akasisitiza kwamba Tanzania inapaswa kuwa ya wote- wanaounga mkono na wanaopinga.

Amesema kuna haja ya kuacha siasa za kukataa ukweli, kuficha matukio na kutoa taarifa za kupindisha majanga. Taifa linahitaji kukiri kwamba kumetokea jambo kubwa, na ni lazima liruhusiwe kuomboleza.

“Wajaluo wanasema ‘binti hawezi kuficha matiti; yakiota yameota’. Tuna msiba mkubwa. Ruhusuni taifa liomboleze. Ni njia ya kuridhiana. Acha fikra za kipumbavu kuhusu dini. Walioua wamo wa dini zote. Hawakutumwa na dini zao kuua. Waliouawa wamo wa dini zote. Hawakufa kwa sababu ya dini zao.”, ameandika.

Katika ushauri wake kwa serikali, Askofu Bagonza amesema ipo haja ya kubadilisha mwelekeo na kuonesha kwamba inasimama pamoja na wale wanaoomboleza. Ameshauri serikali ikiri waziwazi kuwa katika jitihada za kulinda usalama na mali, kuna mambo yalikwenda vibaya, na baada ya tamko hilo, paonekane kwa vitendo hatua za uwajibishaji.

Ameonya kuwa sasa umma ndio unaotoa maoni, na ni muhimu serikali kuwa na msemaji mmoja rasmi anayeeleza msimamo wa nchi badala ya kila mtu kutoa kauli inayoongeza mgawanyiko.
 
Kuna mauvccm, machawa, uwt, wabunge fake, baadhi ya masheikh wa bakwata sa wako busy kughiribu watanganyika waone kama hakuna ubaya uliofanyka kabla na baada ya mo29 tuendelee tu na maisha. Hili halikubariki ni heri tukose wote tu, amani ya maccm waendelee kuua watanganyika, amani ya maccm waendelee kuchota mali za umma na kodi za watanganyika, amani ya maccm kulinda mali zao za wizi, amani ya maccm kuwa madarakan kwa chaguz fake au siyo. Hii haikubariki.
 
“Wajaluo wanasema ‘binti hawezi kuficha matiti; yakiota yameota’. Tuna msiba mkubwa. Ruhusuni taifa liomboleze. Ni njia ya kuridhiana. Acha fikra za kipumbavu kuhusu dini. Walioua wamo wa dini zote. Hawakutumwa na dini zao kuua. Waliouawa wamo wa dini zote. Hawakufa kwa sababu ya dini zao.”, ameandika.
Hakika hapa amesema Kwa hema iliyotukuka 🙏
 
Back
Top Bottom