Askofu Bagonza: Mbowe ameshinda kuliko alivyoshindwa. Tuzo ya Mo Ibrahim inamhusu

Mbowe Ni mchaga na mmachame, mmachame awe 'me' au 'ke' akiona kitu pesa hanaga ndugu, CCM baada ya kulijua Hilo wakatupa Chambo yao ambayo kaimeza na haijamletea madhara na katoka nje ya system kawaachia wengine
Husimchonganishe!!!1
 
Askofu kanena kweli, maana utulivu ulioonekana katika uchaguzi wa chadema mwanzo hadi mwisho, ni hekima ya mwenyekiti aliyetoka. Chaguzi nyingi za vyama vya sisa hasa upinzani huisha kwa vurugu.
 
Assnte Mheshimiwa Askofu Bagonza, hata mimi nasema .... siamini kama mmeshinda lakini sina pa kukata rufaa.. ..

Ushindi kidogo sana kulinganisha na kelele zile.
Kelele zilikuwa kubwa sana ,ushindi kiduchu ,pongezi kwa Lissu
 
Huyu askofu naye kilaza, tuzo za Mo Ibrahim ni kwa ajili ya marais wastaafu wakati Mbowe siyo tu hakuwa rais baali ni kiongozi wa chama aaliyeshindwa kwenye sanduku la kura na king'ang'anizi wa madaraka.
So unadhani baba askofu hajui hicho ulicho kisema? Anajua na anajua why kaandika hivo
 
Huyu mzee kwenye dini nafikiri alienda kwa sababu ya maslahi tu lakini siyo wito wake! Siasa anaipenda sana yaweza kuwa ndio sehemu yake halisi!
Umebahatika kusoma soma maandiko hasa Biblia? Hasa story za manabii? Majority ya manabii sababu ya wao kufa ilikua kukosoa wana siasa, hakuna anacho kikosea Bagonza
 
MBOWE SIYO MUGABE na TUNDU LISU SIYO TRUMP.

Naandika kupongeza. Sina pole za kutoa.

Nawapongeza Mwenyekiti Tundu Lisu na Makamu wake, Mtani wangu Heche. Hata mimi siamini kama mmeshinda lakini sina pa kukata rufaa. Mwaka huu nina bahati sana. Makamu wote wa vyama vikubwa ni watani wangu: Wasira na Heche. Kuna nini hapa? Najiteua kuwa mpatanishi siku wakigombana.

Nampongeza Freeman Mbowe. Ameshinda kuliko alivyoshindwa. Ametufundisha sote. Kukubali matokeo hutokana na mchakato uliojaa uhuru, uwazi na haki. Tuzo ya MO Ibrahim inamhusu lakini iwe na bahasha nzito, siyo kupewa ubao tu.

Nampongeza Mwakajoka na Mnyika kwa kusimamia vizuri uchaguzi usiku kucha. Hakuna kazi mbaya kama kusimamia uchaguzi. Muulizeni Mzee Lubuva! Baada ya pongezi, nibwabwaje haya:

1. Mbowe siyo Mugabe kwa sababu Mugabe hakuwahi kushinda wala kushindwa uchaguzi. Daima aliamua apate kura ngapi.

2. Mbowe siyo Mugabe wala wale wooote waliowahi kukaa madarakani muda mrefu.
  • Nilikuwapo wakati wa JKN; kama angegombea 1985, angeshinda.
  • Nilikuwapo mwishoni mwa Mzee Ruksa, Mkapa, Kikwete, JPM (Atake Asitake), na hata sasa nipo na Mama, Chifu Hangaya. Wote hawa wangegombea baada ya vipindi vyao kwisha, bado wangeshinda! Mbowe ameshindwa na amekubali matokeo. Yeye ni zaidi ya “Bwawa Darasa” la siasa hapa nchini.

3. Mbowe si Mugabe. Jamani! si rahisi kumshinda aliye kitini. Mjinga mmoja wa chama kingine kaniandikia, “Mwamba kaamua tu kumlegezea mropokaji; angeamua kubaki wangemfanya nini?”
Nami nikamjibu, “waulize waliowahi kuamua kubaki. Toka kujadiliwa na Baraza la Mawaziri hadi kutojadiliwa na Baraza la madiwani!” Huko si kuanguka ni kuporomoka. Mbowe kathibitisha umwamba wake.

4. Tundu Lisu siyo Trump. Wanafanana ukali wa maneno si ujinga wa kisiasa. Wote walipigwa risasi, zikawaongezea kura zao. Wapinzani wa Lisu ndani ya CDM wakapuuza risasi zake na kumuongezea huruma. Lisu ni hukumu isiyo na rufaa kwa watawala wanaotumia risasi badala ya hoja. Rudisheni risasi mfukoni, nendeni shule mjifunze hoja. Wamarekani walitumia risasi, sasa wanaongozwa na “kichaa mstaarabu”.

5. Tundu Lisu siyo Trump. Kwa Trump mihimili inajitegemea na ina nguvu. Hapa kwetu, mihimili inamtegemea Lisu aiseemee na kuisimanga. Mmemsahau Spika Makinda? “Mwanangu Lisu, ebu tusaidie tuondoke hapo jamani”. Natamani Tulia atulie mbele ya Makinda apate twisheni ya kufanya kazi na Lisu.

6. Tundu Lisu na Freeman wameelewana. Wapambe wao wamenuniana. Tatizo lilikuwa moja. Tundu Lisu aliwamudu na kuwaendesha wapambe; Mwamba wapambe walimumudu na kumwendesha. Wote wawili ni somo kwetu: Wapambe wanaweza kukuambia wakati gani kuingia uwanjani (Lisu), lakini hawawezi kukuambia wakati gani utoke uwanjani (Mwamba).

7. Mbowe amefuta makosa yake yooote ya miaka 21 kwa kubonyesha kitufe kimoja tu: Kukubali matokeo. Lisu kachukua mkopo mkuuubwa wenye riba kubwa wakati kazungukwa na vibaka. Atamudu kurejesha mkopo huu? Neno kwa Mbowe: Ukistaafu, USTAAFU. Neno kwa Lisu: Mahaba ya kutongozea na kuolea ni tofauti na mahaba ya kuishi katika ndoa.

8. Wanachadema na Watanzania:
Msiyemtaka kaja. Mliyemtaka kaja. Tuna taifa la kutunza na kustawisha. Mambo yetu hayako sawa. Walio madarakani wananungunika. Walio nje wananungunika. Wageni wananungunika. Wawekezaji wananungunika. Tusifanye maridhiano ili hii hali iendelee. Turidhiane kuondoa hali hii. Watawala wa zamu, msipuuze watu kulala sakafuni mlimani City. Kuna kitu ndani yao.

9. Wako wenye mashaka na Lisu. Nami nimo. Tulio na mashaka tuna bahati moja: Hatuhitaji kumharibia Tundu Lisu. Yeye ana uwezo mkubwa wa kujiharibia. Tumuombee.

10. Huu ni mwaka wa uchaguzi. Kwa CCM kumaliza mkutano wake na CDM kuhitimisha uchaguzi wa ndani, taifa linaweza kuwa tayari limempata rais, Chama tawala na Chama Kikuu cha Upinzani. Penye CCM waweza kuweka CDM na penye CDM waweza kuweka CCM bila kuathiri maana ya nisemacho.
HAKI inaunganisha, DHULUMA inaligawa taifa.

Salaam nyingi toka barafu za milima ya Ufaransa na Ujerumani.
Bagonza kila neno lake lina maana zaidi ya 2, ni vyema kutuliza akili kabla ya kusema chochote na ni vyema zaidi kutokusema chochote juu ya aliyoyaandika Bagonza kama huna ufahamu wa falsafa katika maandishi yake.

Kila andishi lake ni chakula cha akili, nimeshiba.
 
Swali, nini mtazamo wake juu ya Mwamba kukalia kiti miaka 20+ na bado akataka tena?
Naomba mnampongeza kwa kushindwa, ilhali alikuwa bado anakitaka kiti.
 
Bagonza kila neno lake lina maana zaidi ya 2, ni vyema kutuliza akili kabla ya kusema chochote na ni vyema zaidi kutokusema chochote juu ya aliyoyaandika Bagonza kama huna ufahamu wa falsafa katika maandishi yake.

Kila andishi lake ni chakula cha akili, nimeshiba.
Kila mtu ana uhuru wa kujadili jambo lolote kwa kadiri ya ufahamu wake.
Na huo ndiyo uhuru wa maoni.
Hiki ulichoandika ni fallacy ya kutaka kuwanyamazisha wanaowaza tofauti wasikosoe.

Ameandika mambo ya kawaida ambayo yako bayana kwa kila mmoja, katumia lugha tamu na poetic presentation, lakini siyo falsafa!

Kutoa maoni baada ya tukio siyo falsafa!
 
Mbowe alishazidiwa alikuwa hana namna.
Na wakumbuke kuwa kile ni chama cha siasa, siyo dola
Angeng'ang'ania mafaraka watu wangemwachia chama.

Sasa sielewi hawa wanaomtukuza mshindwaji wana maana gani. Jamaa alishapoteza kote. Sikio la kufa...
 
Askofu Benson Bagonza anaandika...

"Naandika kupongeza. Sina pole za kutoa. Nawapongeza Mwenyekiti (CHADEMA taifa) Tundu Lissu na Makamu wake, mtani wangu John Heche. Hata mimi siamini kama mmeshinda lakini sina pa kukata rufaa. Mwaka huu nina bahati sana. Makamu wote wa vyama vikubwa ni watani wangu: Wasira (Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara na Heche. Kuna nini hapa? Ninajiteua kuwa mpatanishi siku wakigombana."

"Nampongeza Freeman Mbowe (Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa), ameshinda kuliko alivyoshindwa, na ametufundisha sote. Kukubali matokeo hutokana na mchakato uliojaa uhuru, uwazi na haki, Tuzo ya Mo Ibrahim (Tuzo ambayo hutolewa mara nyingi kwa viongozi wa nchi za Afrika kutokana na uongozi wao bora, uchaguzi wa kidemokrasia na kuheshimu mipaka ya mihula ya kiuongozi) inamhusu lakini iwe na bahasha nzito, siyo kupewa ubao tu."

Pia soma > Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi
Hiyo tuzo kipewe CHADEMA badala ya mtu
 
Back
Top Bottom