Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesisitiza umuhimu wa maadhimisho ya miaka 70 ya Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia kuwa fursa ya kutafakari historia, mafanikio na changamoto za usajili na usimamizi wa jumuiya hizo, hususan katika kulinda uhuru wa kuabudu Nchini.
Akizungumza kuelekea mkutano wa maadhimisho hayo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 28 hadi 30, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam, Askofu Bagonza amesema ofisi hiyo imekuwepo tangu kipindi cha ukoloni na kuendelea kutekeleza majukumu yake baada ya Tanzania kupata uhuru, ikiwemo kusajili makanisa, mahekalu na misikiti.
Amesema maadhimisho hayo ni fursa kwa Viongozi wa dini, Wanachama wa Asasi za Kiraia na Wadau wengine kushiriki mijadala na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha utendaji wa Ofisi ya Msajili, akisisitiza kuwa taasisi hiyo, kama zilivyo nyingine, inaweza kuwa na maeneo yanayohitaji maboresho.
Soma Pia: Askofu Bagonza: Siku hizi kuna chuki kubwa dhidi ya ukweli katika jamii yetu, watu wa kweli wanachukiwa
“Ninatoa wito kwa Viongozi wenzangu, Wanachama wote wa Asasi na vikundi hivi kuhudhuria na kushiriki mjadala wa uhuru na kutoa mapendekezo ya kuiwezesha ofisi hii kufanya kazi yake vizuri,” amesema Askofu Bagonza