The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Anaandika Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Kalikawe Lwakalinda Bagonza kwenye ukurasa wake wa Facebook.
TUTOKE CHUMBANI TULALE SEBULENI
Bibi wa Kijaluo alijiandaa kwa safari ya kwenda mbali kwa miguu. Usiku wa kuamkia safari, alitoka chumba cha kulala na kulala sebuleni. Kisha akajiambia, “hizo hatua nimezikamilisha, kesho nitaanzia hapa sebuleni”.
Taifa letu lina safari ndefu mbele yetu. Tuliishafika mbali. Tumeporomoka na kupitiliza tulikoanzia. Ili tuweze kuanza tena, nawasihi viongozi wetu, tutoke chumbani tulale sebuleni ili kesho tuanze safari. Ebu tujaribu haya:
1. Asimame kiongozi wa kitaifa atamke kukomesha UTEKAJI. Watuhumiwa wakamatwe kisheria. Kutekana ni hulka ya serikali za kihalifu zinazoongozwa na magenge ya Mafia na Madawa ya kulevya. Mtuhumiwa akamatwe, Umma ujue na familia ijue. Taharuki itaisha.
2. Tukipuuza namba 1, tunahatarisha maisha ya maaskari wetu, watu wetu, na hata viongozi na watumishi wa umma. Maaskari na wateule wasio waaminifu wanatumia mwanya wa kuteka kukomoa, kulipa visasi na kujinufaisha. Serikali ikivunja sheria, inawahamasisha watu kuvunja sheria. KUMBUKA: Mama mkwe akikuzingua, unamzingua bintiye.
3. Tumekosana kisiasa; tuwe na mwanzo mpya kwa kufungulia wote waliofungwa kisiasa. Siasa haijaisha, watatenda mengine lakini kwa sasa waachie tuzungumze.
4. Komesha kuwindana mitandaoni. Jamani, eti hata kuwa na VPN kwenye simu ni sumu?! Tunazidi kulipasua taifa kwa kuwindana kama Digidigi.
5. Serikali isiyokubali kushindwa na wananchi wake, haiwezi kumshinda adui wa nje. Baba akiwa mkali sana na kutoa adhabu ya kutokula, mama anawawekea chakula chooni watoto wake watundu. Serikali ikiri kwamba kuna kitu kilienda vibaya na watu wakafa. Bila ukweli wanabaki na donge,
6. Mbwa akiiba kuku, anayelipa faini ni mwenye mbwa. Akiwa mjanja anamkamata mbwa na kumleta kwa mwenye kuku na kumtandika fimbo za kumtosha. Kesi inaisha. Kuku akiishaliwa hakuna cha KUBALI YAISHE. Serikali itafakari na kuchukua hatua kabla mwenye kuku hajadai kichwa cha mwenye mbwa. SIITAMANI SIKU HIYO.
7. Kwa vyovyote vile hakuna adhabu kubwa kwa mwenye mbwa kuishi akimwogopa mbwa wake. Ni hatari zaidi mbwa akitambua kwamba mwenye mbwa anamuogopa. Amani endelevu ni pale mwenye mbwa akijisimamia na kumhakikishia mbwa kuwa madaraka yake hayatokani na mbwa. Naye mbwa atakuwa mbwa bora akitambua kuwa hatima yake iko mikononi mwa bwana wake. TUSIOGOPANE, TUHESHIMIANE.
8. Watu wengi wameihoji tume ya uchunguzi. Ukisikiliza kwa kufumba macho, unasikia ni tume ya kuwachunguza walioandamana. Gari letu limeibiwa, tunalitafuta mfukoni! Umma unasubiri tume ya kuchunguza walivyoandamana, wakafa, kujeruhiwa au kupotea. MIMI BINAFSI, shida yangu ni viapo vyao visivyooza. Juzi nusura mmoja abambikwe uhaini kwa kiapo cha JKT sembuse hawa Majenerali, Ma IGP, Majaji nk? Nitawashangaa wakijiona wako huru.
9. Kwa kuwa tunaamini fedha inashawishi watu kufanya wasichopenda kufanya, basi tuache kutumia fedha katika vikosi kazi vilivyosambaa nchi nzima. Havina uratibishaji mpaka vinavalisha watu misalaba, Rozali na makanzu ya mashehe na kuwaita viongozi wa dini. Tumeishatenda dhambi mbaya ya kuua, tusifanye kufuru kwa kutumia dini kusafisha uchafu wetu. Kuna siku Shehe atapiga alama ya msalaba msikitini
10. Kuna kilio na kijembe kimezoeleka masikioni: Kinahusu watu walio nje kuwa ni wachochezi. Kina kasoro nyingi, nashauri kiachwe.
a). Watu si wajinga kushawishiwa wasichopenda. Kama huamini, nawe washawishi wakufuate wewe.
b). Siyo sifa njema kuwa na wakimbizi nje. Tuifanye nyumba yetu kuwa ya wote - wema na wakorofi.
c). Kubaki ndani si kigezo cha uzalendo. Kuna mijizi, mifisadi, michokoraa, miuza siri za nchi na mirafi imejaa humu ndani.
Mwisho: Tumeumizana na kuliumiza taifa letu. Haitakuwa rahisi kurudi tulivyokuwa. Tunahitaji kuukubali ukweli ndipo tusonge mbele. Tutajidanganya tukifikiri kuwa Baba huwa hashindwi kesi na watoto wake. Gen Z ni kizazi kingine. Naliombea Taifa Langu.
Nawaombea hata waliofika kuniteka wakakuta sipo. Wasikate tamaa, narudi upesi. Kama kutekwa kwangu kutarejesha taifa langu nililolipenda na kulitumikia kwa moyo wangu wote - NIKO TAYARI.