PostGE2025 Askofu Bagonza: Nchi hii hakuna mwenye amani, sio waliochaguliwa au waliopiga kura

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), anayesimamia Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa hapa nchini Tanzania hakuna mwenye amani; si waliochaguliwa, si waliopiga kura, si waliogoma kwenda kupiga kura, wala wasio na upande wowote. Amesema hata waliokuwa wakisimamia uchaguzi hawana amani, akisisitiza kuwa kuna jambo lilienda mrama.

Askofu Bagonza ameeleza kuwa ikiwa uchaguzi utakuwa na kasoro, hakuwezi kuwapo amani, kwa kuwa amani ya taifa hutegemea haki, uwazi na uaminifu katika mchakato wa uchaguzi.
 
Dah!Huyu Mzee anawakomelea Sana misumari ya utosi wadhalimu.Watakuwa wanachukia sana na kutamani wambadilishe awe mishikaki wamtafune kwa mbilimbi.Baba Askofu,strike the iron while hot!
 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), anayesimamia Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa hapa nchini Tanzania hakuna mwenye amani; si waliochaguliwa, si waliopiga kura, si waliogoma kwenda kupiga kura, wala wasio na upande wowote. Amesema hata waliokuwa wakisimamia uchaguzi hawana amani, akisisitiza kuwa kuna jambo lilienda mrama.

Askofu Bagonza ameeleza kuwa ikiwa uchaguzi utakuwa na kasoro, hakuwezi kuwapo amani, kwa kuwa amani ya taifa hutegemea haki, uwazi na uaminifu katika mchakato wa uchaguzi.
Hata police na jeshi hawana amani
 
Tena hata afadhali ya wapiga kura hawana furaha lakini hawana hofu.. Wao wana vyote viwili
 
Ndio shida ya viongozi wa nchi hii!, nchi inaongozwa kwa misingi ya katiba na sheria ila wao ndo wanakuwa wa kwanza kuzivunja sheria na kutokufuata katiba.
 
Huyu faza anapigaga palepale kwenye mshono tena mbichi

Bila haki huwezi kuwa na amani!
 
Back
Top Bottom