Askofu Bagonza (Phd) juu ya anguko la Uchumi Tanzania leo kaandika haya

Askofu Bagonza (Phd) juu ya anguko la Uchumi Tanzania leo kaandika haya

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
UZOEFU TOKA ARGENTINA​

Wiki hii tumepokea ripoti tatu zinazofanana. Kwanza, iliyokuwa hotel maarufu ya Grudoto kubadilishiwa matumizi na kuwa bweni la chuo katikati ya kampeini za kitaifa kuboresha utalii. Kama tujuavyo, utalii unahitaji hotel nzuri.

Pili, mgogoro kati ya kiwanda cha Dangote na benki ya RSK unaotishia kufunga kiwanda hicho muhimu katikati ya uhaba mkubwa wa saruji nchini. Tatu, tangazo la kufungwa kwa kampuni ya New Habari Corporation kutokana na kushuka sana kwa mauzo ya habari. Kama ni kweli, hili ni pigo kwa soko la ajira rasmi na isiyo rasmi katikati ya kilio kikubwa cha ajira nchini.

Siku za karibuni nilitembelea jiji kubwa la Buenos Aires huko Argentina. Niliweka kambi hotel kubwa iitwayo Gradiose Hotel. Ina vitanda zaidi ya 600.

Dakika chache baada ya kuingia chumbani, alikuja Meneja Mkuu na kuomba kuongea nami kwa dakika chache. Aliniambia yafuatayo:

1. Mwenye hotel aliamua kuuza hotel na kuacha biashara kwa sababu ilikuwa inatengeneza hasara.
2. Wafanyakazi wapatao 300 pamoja na watoa huduma kwa hotel (suppliers) waliungana na kufungua kesi kumzuia mwenye hotel kuiuza.
3. Walishinda kesi lakini kwa masharti kuwa wamlipe mwenye hotel fedha anazohitaji kila mwezi.
4. Wafanyakazi na watoa huduma walikutana na mwenye hotel na kukubaliana wao kuendesha hotel na kumlipa kiasi walichokubaliana kila mwezi.
5. Wafanyakazi walikutana na kukubaliana kupunguza mishahara yao na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanabaki kwenye ajira (bora kupata kidogo lakini uwe kazini).
Baada ya kunieleza hayo akaniomba mambo matatu:

1. Kuzima taa kila ninapotoka nje ya chumba.
2. Kubadili taulo na mashuka kila baada ya siku moja badala ya kila siku.
3. Kufunga maji wakati wa kujipaka sabuni ninapooga na ya kuyafungulia ninapoyahitaji tu.

Alisema nikifanya hivyo nitaokoa fedha na ajira za watu. NILIKUBALI akaondoka.
Tunajifunza nini?

Kila mtu afikiri na kutafuta majawabu. Kufunga kiwanda, kufunga hotel, shule, chuo, kiwanda nk si kumkomoa mmiliki. Wamiliki walio wengi tayari wana hela ya kula, nyumba za kuishi, matibabu, na watoto wao wanasoma. Anayeumia ni serikali anayelazimika kushughulika na wahanga wa kufungwa kwa taasisi hizo. Hata wamiliki wakipelekwa jela, itaongeza ajira ya maaskari magereza na order ya bunduki na risasi za ziada

Mkweli kwa Mungu na Taifa langu.

 
Wameziba masikio kwakuwa mishara Yao hakuna wakuigusa, wamefunga macho na masikio ktk ajira maana waatoto wao Wana ajira na nilazima waajiriwe. Wametufunika kilemba cha ukoka machoni wapo Kwa wanyonge Ila Wana tutafuna Kwa maneno yao. Jion inakuja usiku watakao ukumbuka.
 
Tulieni hizo ni changamoto za kawaida kwa nchi za uchumi wa kati, mitambo ikikaa sawa mtaanza kula mema ya nchi
 
This is a meaning of thinker ,bravo Bagonza sio wale wasomi wetu wa kusifia sifia ujinga ujinga unaoendelea ndani ya nchi,Tanzania ni yetu sote sio mali ya kikundi fulani cha watu.
 
Mitano tena,,,,,,,,!!
Na bado
Mashirika ya Habari yanafungwa kwa sababu ya kuchapisha propaganda badala ya Habari
 
Tutapeleka jeshi litazalisha Cement, litaandika habari na kuchapisha. Kwa upande wa Ngurdoto ndiyo kama mlivyoona, wakishindwa wanafunzi tukabidhi kwa jeshi.
 
Bagonza aisee.....
Usimshangae pengine sababu ya kufungwa Ngurudo hajui chanzo chake, kufungwa kiwanda cha Dangote ametaja moja tu na zingine hazijui na Gazeti kufunga biashara
Hiyo historia ya wauzaji wa Magazeti siku zote hajazijua. Angeenda kwenye kila moja akataja sababu iliyosababisha bila ubabaishaji najua atataja kodi bila kuchunguza sababu zilizosababisha atakuwa basi anasimulia alichokiona bila kuhusisha na kulinganisha na yanayoendelea kwa makampuni aliyoyataja ya hapa nchini.
 
Back
Top Bottom