Askofu Bagonza: Siku hizi kuna chuki kubwa dhidi ya ukweli katika jamii yetu, watu wa kweli wanachukiwa

Askofu Bagonza: Siku hizi kuna chuki kubwa dhidi ya ukweli katika jamii yetu, watu wa kweli wanachukiwa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


​
Askofu wa Kanisa la Evangeliki la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza, amewataka viongozi kuheshimu na kuwajali watu wanaowaongoza badala ya kulewa madaraka. Akizungumza Agosti 31, 2026, katika ibada iliyofanyika Dayosisi ya Mwanga, Askofu Bagonza alisisitiza kuwa kigezo kikuu cha kupima uongozi bora ni jinsi kiongozi anavyowatendea na kuwaheshimu watumishi au wananchi walio chini yake.

Askofu Bagonza alibainisha kuwa nafasi za uongozi ni za utumishi na uwajibikaji, hivyo kiongozi anapowaumiza au kuwanyanyasa walio chini yake, anawasaliti na kumuumiza Mungu aliyeweka dhamana hiyo mikononi mwake.

Hali kadhalika, alikemea tabia ya jamii na baadhi ya viongozi kuchukia ukweli na kuwatenga watu wakweli. Alifafanua kuwa ingawa ukweli ndio sifa kuu inayomfanya mtu apewe uongozi, mara nyingi viongozi wakishapata madaraka huuchukia ukweli huo na kujizungushia wasaidizi wanaowadanganya, jambo linalobomoa mambo mema yaliyojengwa kwa gharama kubwa.

"Siku hizi kuna chuki kubwa dhidi ya ukweli katika jamii yetu. Watu wanauchukia sana ukweli. Ukweli unachukiwa na wa kweli wanachukiwa. Watu wa kweli katika jamii yetu ni wapweke na ni masikini" -Amesema Askofu Bagonza
 
Back
Top Bottom