The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasawake wa Facebook.
MGAWANYO WA MAJUKUMU TUUHESHIMU❗️❗️❗️❗️
Ofisi ya Msajili wa vyama siasa inaonekana kuwa na majukumu mengi. Yapo yaliyoandikwa katika sheria, na mengine hayajaandikwa. Ili kuyaelewa yote inabidi utumie hekima. Mara nyingi sheria isiyoandikwa ina nguvu kuliko iliyoandikwa.
Kwa maoni yangu, kuna mgawanyo wa majukumu katika ofisi hiyo. Tunaalikwa kuheshimu huo mgawanyo. Inawezekana mgawanyo huo ukawa uko hivi;
1. Jaji Francis Mutungi ndiye Msajili wa Vyama vya siasa. Hii ni kazi ya jumla.
2. Ndugu Sisty Nyahoza ni Msajili wa Chadema. Kwa ajili “upekee” wa chama hicho, kinahitaji Msajili maalum.
3. Mgawanyo huu unazalisha tunda lisilotegemewa. Mmoja anajenga na mwingine anabomoa.
4. Wote bila kujua, wanaihujumu mamlaka iliyowateua ama kwa kukosea kuelewa maelekezo au ujuzi mdogo katika kutekeleza walichoelekezwa.
5. Wanavionea vyama vingine kwa kutumia muda na raslimali nyingi kushughulika na chama kimoja tu. Kwa njia hiyo wanakijenga na kukinadi kila wakati kwa gharama za vyama vingine.
Wajaluo waligundua mapema wakawaonya watoto wao waache kuchamba sana. Hatari yake waliibaini mapema sana.