Askofu Bagonza tafuta miafaka ndani ya KKKT kabla ya kuingilia masuala ya siasa

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Inashangaza kuona kiongozi wa dini ambaye ni muasisi wa mgogoro uliopo ndani ya kanisa la KKKT katika jimbo la Konde.

Ambapo ya baada Askofu Dk Edward Mwaikali wa Jimbo la Konde kuondolewa katika nafasi yake na uongozi wa kanisa hilo kutokana na sababu za kiutendaji, Askofu Bagonza aliifanya kuwa anaingilia suala hilo kwa lengo la kulisuluhisha huku nyuma ya pazia akiandaa njama chafu kwa kushirikiana na Askofu Mwaikali ya kuyapoka/kuyagawa baadhi ya majimbo ya kanisa hilo ili kuleta mpasuko na migogoro zaidi ndani ya Kanisa la KKKT.

Hivyo ni jambo la ajabu na kustaajabisha kuona muasisi wa mgororo ndani ya Taasisi ya kiroho kupaza sauti bila haya usoni kutaka Miafaka katika masuala siasa chini.

Askofu Bagonza nakukumbusha mstari huu wa biblia;

Mathayo 7:5

Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako.

Na Yothan Mwakipesile
Rungwe-Mbeya.
 
Kati ya Job Ndugai na Tundu Lissu je ni nani mtoro bungeni na hajulikani aliko?
 
Bagonza ni mtu wa fact na si porojo za njaa kama hizi.

Bagonza ni akili kubwa. Huwa hajibizani na mtu(personal attacks)

Inahitajika akili kubwa kujibizana na Bagonza na si elimu kubwa.

Narudia tena.....kujibizana na Bagonza uwe na akili kubwa na si akili za njaa kama hizi.
 
Bagonza na Shoo wamegeuza makanisa kuwa maduka yao binafsi ya kupiga Hela, pia wamegeuza makanisa kuwa Ofisi za Chadema na kufanyia udalali wa kisiasa.

Wanakopa fedha benki kwa dhamana ya kanisa Kisha wanawapa fedha hizo Chadema, ndicho kilichotokea Konde, sehemu nyingine zitalipuka taratibu.

Mwaikali kawagomea maana anawajua, walitaka kuuza hoteli ya matema beach, Mali ya kanisa Kisha wainunue kwa mgongo wa nyuma iwe yao, walishaandaa mpaka wateja
 
Huyo askofu hata wanaomwamini akili zao zinapaswa zipimwe , mbna hata body gesture yake tuu anaonekana huyo sio ngano Safi Bali magugu
 
Boganza ana haki ya kukosoa bila kujali yeye binafsi ana matatizo gani kama hamtaki kukosolewa achieni ngazi

Mnapoambiwa ukweli mnaanza kuattack
Watu personal how?
jibuni hoja za watu acheni porojo hizi ni porojo unalete hapa

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Qwy
Ila waprotestant migogoro ndani ya kanisa Ni Kama ibada..Tumechoka, viongozi badilikeni
 
Wanachato mkisikia jina bagonza mnapataga kichefuchefu kama waja wepesi!!
 
Tanzania ni bora kuliko KKKT
 
Bagonza ni kiongozi wa kiroho (askofu), lakini yeye mwenyewe ni mtu wa mwilini; masuala ya watu wa rohoni hayawezi kusuluhishwa na watu wa mwilini. Bagonza na Shoo wajitoe kwenye kusuluhisha mgogoro wa KKKT Konde.
 
Bagonza mnafiki wa kupindukia.
Ndio wale wanaokula vipande 30 vya fedha.
 
Nyie watu wa Rungwe mna shida.
 
Wajinga kama ninyi mnafikiri hivyo.
Bagonza ana tuhuma nyingi za tamaa za mali, vyeo na hata mwilini kwa kuwa na watoti wa nje.
Hili la kumpa sapoti uasi wa Mwaikali kaingia choo cha kike.
 
Kanisa ni KATOLIKI TU haya mengine ni ujanja ujanja
 
Mnafiki hawezi kuendeleza Neno la Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…