Askofu Bagonza: Tunahitaji nguvu ili kuharibu

Askofu Bagonza: Tunahitaji nguvu ili kuharibu

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
TUNAHITAJI NGUVU ILI KUHARIBU.

Mzee Malecela aliwahi kusema, “urais siyo kubeba karai la zege”. Alimaanisha uongozi hauhitaji kutumia misuli na mitulinga. Mara nyingi tunahitaji kutumia nguvu ili kuharibu. Ili kujenga, kupatanisha, kutenda haki, kuridhiana na kutunza amani, tunahitaji HEKIMA TU.

Suala la Ngorongoro linajitaji hekima, si nguvu. Linahitaji kushindwa si kushinda. Linajitaji kujishinda si kuwashinda wengine. Linahitaji kusikiliza watu (si washauri) kuliko kusema.

Nilichelewa kuilaumu serikali na nitachelewa kuipongeza. Kwa nini?

1. Rais alikuwa anahubiri 4R wakati watendaji wa serikali wakitumia misuli, hila, mizengwe, wasanii, na wana habari ndumila kuwili. Najua nakosea kumtenga rais na serikali yake lakini nafanya makusudi ili kuwaonya watendaji wasiojielewa. Ipo siku watageuka nyuma wakute rais hayupo.

2. Suala la Ngorongoro linatishia kuchafua usafi wa mihimili na vyombo
vingine nyeti. Tusitishe matumizi ya nguvu na kuondoa pazia za usiri ili kudumisha amani. Watu wema hufurahia nuru. Waovu hupenda giza.

3. Wateule wa Rais waliotumwa kupeleka habari njema Ngorongoro amekosekana mmoja wa TAMISEMI. Kura ndilo daraja kati ya wananchi na watawala wetu. Bila kura, serikali inakosa uhalali wa kuwaambia chochote wananchi. Daraja hilo (TAMISEMI) limedhohofika. Tufikiri upya katika muktadha wa maridhiano. Imani ikikosekana, hakuna njia ya kuonekana haki inatendeka.

4. Kama Ngorogoro pametulia, Rais ageuze shingo na kutazama mahali pengine panapofuka moshi. Tumtibu njiwa akiwa bado na uwezo wa kuruka. Kuna mioshi maeneo mengi na nguvu haifai tena. Hekima tu ndiyo inahitajika kurejesha imani ya wananchi kwa watendaji.
 
Wakiondolewa chawa wanasifia, wakiachwa wabaki chawa wanasifia , chawa ni chawa tu.
20240716_084757.jpg
 
Back
Top Bottom