Askofu Bagonza: Ujinga ni mtaji

Askofu Bagonza: Ujinga ni mtaji

Anaandika Askofu Bagonza

Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:

1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.

2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.

3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.

4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.

5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.

6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.

7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.

8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.

9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.

10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.

Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.

NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii
Hii iwekewe lamination kabisa
Ili wale viongozi wa wa wajinga wasije wakaichana kwa hasira kwa wajinga wao kuambiwa ukweli

Walau tuna chuo kilichotoa PhD
 
Anaandika Askofu Bagonza

Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:

1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.

2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.

3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.

4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.

5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.

6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.

7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.

8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.

9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.

10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.

Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.

NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii
Ni kweli na pia Ni ujinga Kuomba ufadhali kuwafundisha watu elimu ya watu wazima kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK)
 
Ndio maana figisu zilitumika Sana kutoka kwenye mamlaka za kidunia hata Kama Ni kuvunja katiba ya KKKT ili huyu mwamba asiwe askofu mkuu wa KKKT .
Wangekuwa na uwezo wangetamani hata maaskofu Katoliki waingilie mchakato,lakini uzuri ni kwamba Huwa wanayeuliwa kuto Vatican makao ya RC.
Leo tungekuwa na kadinari mwenye kuungwa mkono na White House.

BAKWATA ipo mfukoni 😅😅
 
Askofu Bagonza: "Ujinga ni Mtaji"?
Alama ya kuuliza nimeiongeza.

Binafsi siamini kuwa ni "Ujinga". Hivi mtu anaweza akaachana na ujinga kwa kipindi fulani, halafu baadae akauokota tena ujinga ambao alikwisha achana nao?

CCM haitumii "ujinga" wa waTanzania, bali ilicho kifanya ni "KUWAFANYA WATANZANIA KUWA MATEKA.
Wewe fikiria hata sehemu ambazo huwezi kutegemea kuwepo wajinga; kwa mfano ndani ya kundi kama TLS (Tanganyika Law Society)' lakini kundi hili nalo limetekwa. Shuhudia wanavyo lazimishwa kuwapata viongozi wao kwa kuondolewa wasiotakiwa na CCM.

Hata huko ndani ya dini, CCM imejiingiza na kuwapata mateka. Viongozi wengi huko huwezi kuwaita kuwa ni wajinga, lakini wanatekwa kwa njia mbalimbali, wengine hata kupewa rushwa (milioni kumi zawaidi ya siku ya kuzaliwa kiongozi wa dini. Huku ni kutekwa, kama kiongozi huyo akikubali, siyo amegeuka na kuwa mjinga.

Mateka atajinasua vipi kutoka katika hali yake ya umateka?
Hili ndilo linalopaswa kujadiliwa kwa kina, hasa wakati huu tunapoelekezwa tuendelee kuukubali umateka wetu kwa kuwarudisha CCM kuendelea na utekaji wao.

tukishindwa kujinasua safari hii kwa amani, italazimu tuukate huu mnyororo wa umateka wetu kwa kumwaga damu ya waTanzania. Huko ndiko inakotupeleka CCM.
Kuruhusu kutekwa na mtekaji mwenyewe hata hatumii siraha ya moto bado ni ujinga tu. Siku zote mtekaji hawezi kumteka kienyeji enyeji mtu anayejielewa. Mfano mzuri ni hizo taasisi mbili ulizotolea mfano, viongozi wa dini kuruhusu kutekwa ni ujinga, TLS kuruhusu kutekwa ni ujinga pia. Kwa hiyo ujinga ndio tatizo hapo
 
Bila wajinga kuwepo wajanja hatuwezi kuishi wacha waendelee kuwepo kwani wajinga ndiyo waliwao. Na heri kuwa mjinga kuliko mpumbavu.
 
Anaandika Askofu Bagonza

Tulizoea kusema UJINGA NI MZIGO lakini kwa sasa UJINGA NI MTAJI wa makundi mbalimbali:

1. Viongozi wa Dini: Wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.

2. Wanasiasa: Wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.

3. Waganga wa kienyeji: Wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.

4. Walimu: Wanajitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.

5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu: Wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.

6. Wahisani na Wafadhili: Wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.

7. Serikali: Inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.

8. Matapeli wa Mitandaoni: wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.

9. Wafanya biashara: Wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.

10. Umaskini na Maradhi: Wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.

Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.

NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii
Labda tuchague Rais mjinga ili naye ateue Mawaziri wajinga; hapo wananchi werevu watawamudu!
 
Lakini si ni Mungu alieiumba dunia na Ujinga uliyomo, Kwenda kanisani na kutoa Sadaka ni ujinga pia atusisitize hilo Askofu.
 
Kuruhusu kutekwa na mtekaji mwenyewe hata hatumii siraha ya moto bado ni ujinga tu. Siku zote mtekaji hawezi kumteka kienyeji enyeji mtu anayejielewa. Mfano mzuri ni hizo taasisi mbili ulizotolea mfano, viongozi wa dini kuruhusu kutekwa ni ujinga, TLS kuruhusu kutekwa ni ujinga pia. Kwa hiyo ujinga ndio tatizo hapo
Hapana. Bado huelewi.

Hawa wote hawatekwi bila ya nyenzo kutumika. Nyenzo kuu ni 'Vyombo vya Dola'. Kuna nyenzo nyingine nyingi zinazotumika, lakini hiyo moja ndiyo kuu.
Ondoa hivyo vifaa leo hii, utaona jinsi CCM itakavyo sambaratika.
CCM sasa hivi ni dubwanda tu lililoshikiliwa pamoja na nguvu hafifu sana. Hii ikiondolewa hutaamini kuona hawa washenzi wanaojidai leo kuwa CCM damu damu wakilikimbia dubwasha hilo.
 
Back
Top Bottom