Tulizoea kusema ujinga ni mzigo lakini kwa sasa ujinga ni mtaji wa makundi mbalimbali :-
1. Viongozi wa dini wanahitaji wajinga wengi ili wawauzie wokovu, utajiri hewa, uponyaji nk.
2. Wanasiasa wanahitaji wajinga wengi ili wawadanganye bila kukamatwa na wawajaze ahadi hewa.
3. Waganga wa kienyeji wanahitaji wajinga wengi wa kuwaletea kuku huku hao wajinga wakilishwa vinyesi na mikojo.
4. Walimu wanahitaji wajinga wengi ili wafanye mazoezi ya kufuta ujinga kwa kuuongeza.
5. Watumishi wa serikali wasio waaminifu wanahitaji wajinga wengi ili wawatoze rushwa na kuwauzia haki zao.
6. Wahisani na wafadhili wanahitaji wajinga wengi ili wapate pa kupeleka misaada inayodumaza na kuwasaidia kumiliki uchumi wa wajinga.
7. Serikali inahitaji wajinga wengi ili waiogope. Kwa kawaida serikali huwaogopa wananchi wanaojielewa.
8. Matapeli wa mitandaoni wanahitaji wajinga wengi ili waweze kutajirika bila kufanya kazi.
9. Wafanya biashara wanahitaji wajinga wengi ili wanaoamini kuwa kuna duka la bei nafuu.
10. Umaskini na maradhi wanahitajika wajinga wengi ili hawa ndugu waendelea kustawi.
Vita ya kupambana na ujinga haijaanza. Ikianza mniamshe. Hakuna kundi lisilo na mjinga. Ukichunguza kundi usimuone mjinga, tambua wewe ndiye mjinga.
NB: Mimi mniamshe siku mkimuona kiongozi yoyote anapambana watu wake waache ujinga kwenye nchi hii.