Anaandika Askofu BENSON BAGONZA (PhD)
CCM HONGERA SANA: Mmekula Ng’ombe mzima, Msishindwe kula mkia.
Kwa moyo wa dhati nawapongeza CCM kwa kuitisha na kuendesha Mkutano Mkuu Maalum kwa mtandao. Nawapongeza zaidi kwa kufanya mabadiliko madogo (kwangu ni makubwa) ya katiba ili kuwapa viongozi madaraka makubwa zaidi ya kufanya kazi.
Kwa tukio hili CCM wametuonyesha mambo matatu:
A. Katiba si msahafu. Ni nyenzo ya kufanyia kazi. Nyenzo hii inaweza kurekebishwa wakati wowote ili kukiwezesha chama kufikia malengo yake.
B. Chama kina uhuru wa kuendesha mambo yake kinavyotaka.
C. Chama kinaongozwa na imani. Kinaweza kuchukiwa na watu wengine lakini wenye chama na wenye imani nacho wanao uhuru wa kukipenda na kukisimamia.
PAMOJA na pongezi zangu kwa CCM, navutwa kuwasihi na kuwakumbusha yafuatayo:
1. Uhuru wa wana CCM kwa chama chao unatakiwa na wananchi wengine katika vyama vyao. Siasa na dini vinaongozwa na imani na kwa hiyo uhuru wa kuabudu ni sawa na uhuru wa kisiasa kwa watu wote. Waacheni wengine wafurahie vyama vyao kama mnavyofurahia chama chenu.
2. CCM iliona kikwazo katika katiba yao; WAMEKIONDOA. Wananchi wanaona vikwazo katika katiba ya nchi na sheria za uchaguzi. Wanadai viondolewe. Kwa nini kuahirisha marekebisho hayo mpaka baada ya uchaguzi wakati mnajua yana kasoro? CCM haikufungwa na muda kubadili katiba yake; kwa nini inasingizia muda kurekebisha kasoro za katiba na sheria za uchaguzi?
3. CCM ni chama kilichosajiliwa. Kikubali kuwa chini ya Msajili kama vyama vingine vilivyo chini ya msajili. Kuna raha yake kuwa chini ya Msajili. CCM ina upweke kuwa juu ya Msajili. Ikitaka mshikamano na umma ije chini au iruhusu vyama vyote viwe juu ya Msajili.
4. CCM ni ya wanachama wake lakini inatutawala sote na raslimali zetu. Daima, CCM ikumbuke ukweli huu na ijue haina uhuru wa KUTOWASIKILIZA wasio wana CCM. Yaweza isiwasikilize kwa hasara yake yenyewe.
5. Mataifa hustawi katika msingi wa HAKI au MATUMAINI kuwa haki itatendeka. Taifa likikosa yote mawili ni balaa. Hapa kwetu, hatuna tatizo la AMANI. Tuna deni la HAKI na matumaini yanayotoweka kwa kasi. Tusipuuze, tutapuuzwa.
6. Ushahidi wa namba 5 juu, ni pale unapoona watu mashuhuri wakijitenga na maamuzi ya chama au serikali. Wengine wengi wamegeuka “mabubu mamboleo”. Unaweza kutamani kutukanwa kuliko kukaliwa kimya!
7. Kama wanaojitenga na maamuzi ya chama na serikali wataitwa WASALITI, tujihoji kwa undani. Kama ni WAZALENDO, CCM itumie fursa hii kujirekebisha. Kipimo halisi cha Uzalendo na Usaliti, kiwe ni dhamiri safi, siyo kufuata mkumbo maana hata wengi wanaweza kukosea.
8. Tuking’ang’ania kuwa ni WASALITI, tujiulize wasaliti wakiwa ni watumishi wa “vyombo”, madaktari, marubani, wapishi, madereva, Majaji nk itakuwaje? Tuache kutumia neno hili vibaya. Lina gharama chungu. Tofauti za maoni si usaliti wala uhaini.
9. CCM sikivu itatuzalia serikali sikivu. Kuna maisha baada ya uongozi na kuna maisha baada ya CCM kutawala. CCM ya sasa ikiweka uwanja sawa kwa vyama vyote, asilimia 50 ya matatizo yake ya ndani yatayeyuka. Itakuwa imara kuliko 1977. Imekosa mchawi nje, inamtafuta ndani na wachawi waandamizi ni viongozi.
10. Kwa kufanikiwa kuendesha mkutano mkuu kwa njia ya mtandao (Kinyume na kanuni namba 17 ya sheria ya vyama vya siasa), CCM imeonyesha kuwa palipo na utashi wa kisiasa, kila kitu kinawezekana. Uhuru ilio nao CCM wa kuvunja kanuni hiyo namba 17 ya Msajili wa vyama vya siasa, unahitajika kwa vyama vingine vyote.
Kwa mara nyingine nampongeza Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan. Usawa wa kisiasa ni DENI linalomkabili. Ana uwezo wa kulilipa na kubakiza chenji.