Pre GE2025 Askofu Bagonza: Ushahidi wa Marko Ng'umbi unasambaratisha uhalali wa TAMISEMI na tume “huru” kusimamia chaguzi kwa uhuru na haki

Pre GE2025 Askofu Bagonza: Ushahidi wa Marko Ng'umbi unasambaratisha uhalali wa TAMISEMI na tume “huru” kusimamia chaguzi kwa uhuru na haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Marco na Nape wameudhihirisha umma wa watanzania kwamba CCM wakisaidiana na dola wamekuwa wakipora chaguzi zote nchini.
Hii ni aibu kubwa!!
 
Bagonza lini aliliongelea la wale viongozi wa dini WALIOMCHUNA NGOZI kiumbe dhaifu kabisa....yule mtoto wa Kagera...so sad
 
Askofu Bagonza

"Jumapili ya 1 September mosi 2024, mmoja wa watekaji wa 4R alijitokeza hadharani na kutoa siri kuwa alihusika katika kuvuruga Nchi na kufanya uhaini wa serikali dhidi ya wananchi, ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido anayeitwa Marko Henry Ng'umbi, Rais ametengua uteuzi wake ndani ya masaa lakini ni vyema tukatafakari ushahidi alioutoa kwa kina

1. Kwamba, madiwani wote wa wilaya hiyo walipitishwa bila kupingwa kwa njama za serikali. Hawana uhalali (Legitimacy). Je madiwani haramu waweza kutunga sheria halali katika Halmashauri zetu?

2. DC Mtenguliwa anakiri kushiriki operesheni za maporini katika wilaya kadhaa. Je zilikuwa zipi hizo? Haziwezi kuwa za kuiba kura kwa sababu madiwani walipita bila kupingwa. Jinai haiozi; utenguzi ufuatwe na uchunguzi.

3. Kama DC katenguliwa kwa kusema uwongo, taifa haliko salama. Kama katenguliwa kwa kusema ukweli usiotakiwa kusemwa, taifa haliko salama zaidi. Ukweli na uwongo wa DC Mtenguliwa ndicho kiini cha kifo cha 4R.

4. Walioteka 4R na kuzikataa sirini na hadharani, hawawezi kumpenda kwa dhati muasisi wa 4R. Wanaochukia 4R hawawezi kuwapenda watu wanaonufaika na 4R. Kutekana, kutesana hata kuuana maporini ni matokeo ya kuzichukia 4R na muasisi wake. Hata ndani ya serikali na chama tawala, wapenzi wa 4R wako hatarini.

5. Ushahidi wa DC Mtenguliwa unasambaratisha uhalali wa TAMISEMI na tume “huru” kusimamia chaguzi kwa uhuru na kwa haki kwa sababu mapori yapo. Tusishupaze shingo. Naona msururu mrefu wa wanaosubiri kumwaga siri zaidi.

Najiuliza: Nani alimrekodi na kurusha clip hii? Hiyo pia ni dalili ya ugomvi ndani ya chama na serikali kati ya watekaji na watetezi wa 4R.

Mheshimiwa Rais asiishie kutengua waropokaji. Hata KM wa chama asiishie kukanusha wanaojinadi kuteka au kutishia kutumia dola kukimbia na masanduku.

Kinachowawasha waropokaji hatukijui lakini kwa hakika waropokaji hawa ni maadui wa CCM kuliko wapinzani.

Pia soma
Mahakama zetu zitaamua kwa haki kweli? Angalia ile kesi ya utekaji imeishia je?
 
Serikali isipokuwa makini tunapoelekea kwenye chaguzi kuna uwezekano wa kuliingiza Taifa kwenye shida.
Inasikitisha sana Viongozi kueleza hadharani uchafu waliyotenda kinyume cha maadili na sheria za nchi.
Tuwashukru kwa kueleza ukweli unaoumiza lakini mamlaka za uteuzi zijue kutengua tu hakutoshi ni vizuri wakaruhusu sheria ichukue mkondo wake kupata haki.
 
Back
Top Bottom