Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
VITA YA KAGERA Vs CORONA
Wakati wa vita ya Kagera, Baba wa Taifa akiwa Rais wa Tanzania, alilazimika kufanya mabadiliko ya uongozi wa Mkoa wa Ziwa Magharibi. Mkoa huu ulikuwa katika eneo la msitari wa mbele vitani. Alimuondoa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa na kumteua mwingine anayendana na mabadiliko na hali halisi ardhini.
Mkuu wa mkoa aliyekuwepo alikimbilia kuhamisha familia yake na kutumia muda mwingi kuangalia usalama wake na wa familia yake.
Sasa tuko vitani na KIRUSI cha CORONA. Vita haina macho lakini kanuni za vita hazibadiliki.
Nasihi, nashauri, kanuni za vita zifuatwe. Uongozi wa makamanda ni muhimu kuliko ubora wa silaha.
Hekima ya Wanyambo inasema, "unaweza kumpenda sana binti yako lakini huwezi kuondoka naye kwenda kuolewa alikoolewa".
Tuko vitani DSM, kamanda asiyepunguza majeruhi wa vita, hatufai, hamfai jemedari Mkuu na anafaa kwa kuwasaidia maadui wetu.
Tusichelewe kama tulivyochelewa kusoma alama za nyakati. Hata kichaa ana jambo la kutufundisha.
Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe. Anayekataa kuambiwa jambo, hawezi kukataa kuona madhara ya kukataa kwake jambo hilo au kukataa kuona madhara ya jambo lenyewe.