Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Askofu Bagonza akihubiri katika Ibada ya kuweka Wakfu Vifaa na Alama za Kanisa zitakazotumiwa na Askofu Mteule wa Dayosisi ya Mwanga, amesema.
Wafalme wabaya na watawala wabaya ili wafanikiwe, huwa wanaanza kuchafua hekalu. Hekalu likishashachafuka na kudhoofika, unabii hukoma, na wafalme dharimu hupata nafasi ya kufanya watakavyo kwasababu hakuna atayediliki kutoka katika hekalu chafu kumsema mfalme.
Ukitaka kujua hali ya Taifa lolote, tazama yanayofanyika hekaluni, ukiona wizi wa sadaka kanisani, ujue nje ya kanisa pananuka zaidi. Ukiona uongo na dhambi nyingine chafuchafu zinatamalaki ndani ya hekalu, ushirikina, ubadhirifu ndani ya hekalu, nje ya hekalu hapatamani. Au badilisha, badala ya hekaluni anzia duniani. Ukikuta madhambi yanapepea pekupeku huko duniani ujue chanzo chake ni hekaluni.
Tunaweza tukatoa pepo sana, tunaweza tukatoa sadaka sana, tunaweza kufunga ndoa za kifahari, tunaweza kuwa na ufahari sana, lakini matengenezo ndugu zangu ni zaidi ya ukisasa, yanaanzia rohoni kwanza kabla ya kwenda nje. Matengenezo yanayoaanzia nje kuja rohoni hayawezi kudumu.
Mtume Paulo nasema Miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu, tena tumeagizwa kama kanisa kuwa walinzi na walezi wa dhamiri za waumini wetu, ndio hatutendi dhambi, ndio wewe binafsi ni msafi, lakini usafi wako binafsi si kitu ikiwa macho yako hayaoni uovu, na midomo yako imefungwa isikemee ndani na nje ya hekalu. Hayo yote yamekushinda, umeshindwa kukemea, umeshindwa kuonya, hata kununa umeshindwa? Nuna basi tukuone umenuna kwa ajili ya mambo mabaya yanayotokea katika jamii.