DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), anayesimamia Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa wahusika walijua mapema kuwa watatenda makosa, kwa lengo la baadaye kusema tufanye maridhiano, na kwamba walichokikusudia tayari kimeshatekelezwa. Kwa mujibu wake, changamoto kubwa iliyopo sasa ni swali la msingi, maridhiano hayo yafanyike kati ya nani na nani?.
Askofu Bagonza amebainisha kuwa amewahi kutembelewa na wageni kutoka Arusha waliomweleza kuwa bado wako katika hali ya mshtuko (trauma) kwa sababu hawajapata fursa ya kuwazika ndugu zao waliopoteza maisha. Amehoji kuwa haiwezekani kuzungumzia maridhiano ya kweli wakati bado kuna watu ambao hawajapata haki ya msingi ya kuomboleza na kuwazika wapendwa wao, akisisitiza kuwa maridhiano ya dhati hayawezi kujengwa juu ya maumivu ambayo hayajatibiwa.