Askofu Bagonza: Walioua na waliouawa si Walutheri tu. Hata waliofanya maamuzi ya kuua siamini kama ni Walutheri

Askofu Bagonza: Walioua na waliouawa si Walutheri tu. Hata waliofanya maamuzi ya kuua siamini kama ni Walutheri

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Tafadhali tuliza akili unaposoma makala hii.

1. Kuna mjadala unaendelea kuhusu dini zetu na sasa KKKT inatuhumiwa sana. Kanisa linahusishwa na siasa za urais, kulambishwa asali na misimamo ya watu binafsi lakini Walutheri inaelekea kutumiwa ili kupata upenyo wa kulikashifu kanisa zima. Tunavuka msitari mwekundu bila sababu.

2. KKKT ni taasisi ya umma. Linajadilika na kushtakika LAKINI lisikashifiwe bila hoja wala ushahidi. Askofu Bagonza akibaka, akiiba, akipokea rushwa - si KKKT iliyofanya hayo. Shughulika na Bagonza, achana na kanisa. Kumbuka kanisa lina u-Mungu na ubinadamu.

3. Kwa muundo wake na katiba yake, msimamo wa KKKT unatokana na mapatano ya vikao WALA si maamuzi ya kiongozi. Hatujakaa na kwa hiyo hatujawahi kupatana lolote kuhusu siasa za nchi. Kama kutopatana ni kosa, tunalikubali.

4. Kwa kuwa vikao huitwa na viongozi, INAWEZEKANA kumteka kiongozi na kumfanya asiitishe kikao na kanisa lionekane halina msimamo. Kutokuwa na msimamo rasmi ni msimamo kama ni kanisa limeamua kutokuwa na msimamo kama lilivyo sasa. Litajibu kwa Mungu na “ikibidi”, kwa wanadamu.

5. Baadhi ya viongozi tumekuwa na kimbelembele cha kutoa maoni kuhusu siasa za nchi. Kama maoni hayo yanatokana na kupewa au kunyimwa asali, bado ni maoni yetu binafsi si ya kanisa. KKKT hatujawahi kukaa kupanga rais awe Mlutheri! Kanisa liheshimiwe.

6. Katiba ya nchi haizuii Mlutheri kuwa Rais. Siyo dhambi wala ajabu Mlutheri kuwa rais. Katiba haimilikishi urais kwa dini wala dhehebu fulani. Kama kuna wanaoutaka watazamwe kwa sifa zao si kwa madhehebu yao au wasinyimwe kwa sababu ya dini zao na madhehebu yao. Ifahamike, matatizo yanayolikabili taifa letu hayakuletwa na Ulutheri.

7. Utekaji, ubabe, rushwa, kukosa ajira, kupuuza haki na kuimba amani, udhaifu wa utawala wa sheria, kuminya demokrasia na wizi wa kura, vimewapiga upofu watawala wetu, kisha wakawadanganya watu kuanza kutazamana dini na madhehebu yao badala ya kutazama changamoto za nchi. Haya yote hayakuletwa na Ulutheri lakini sasa yanatumiwa kuliondoa taifa kwenye kiini cha tatizo. Acheni ushirikina.

8. Kudai Walutheri ni bora kuliko Wakatoliki ni uchochezi. Fimbo inayomtandika Mkatoliki leo, kesho itamtandika Mlutheri. Keshokutwa Walutheri na Wakatoliki wataungana kumtandika Muanglikana au Mwislamu anayeweza kuwa anajiona bora sasa. Tumefilisika kupita kiasi. Serikali bora ni ile inayoona fahari kushindwa na wananchi wake kuliko kuwashinda kwa hila.

9. Narudia kusema: Hakuna chama cha kushinda urais peke yake. Hakuna dini wala dhehebu moja peke yake linaweza kushinda uchaguzi. Hata “dhehebu” jipya linaloitwa “vyombo” linahitaji kura za risasi, pingu, mabomu na asali ili kushinda urais kwa muda mfupi tu. Tunahitaji maridhiano yaliyojengwa katika UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI. Wanaokataa hili ni wapiga dili kwa kisingizio cha KAZI MAALUMU.

10. Bila maridhiano, kufukua makaburi hakutaisha hata ndani ya chama tawala. Sasa linafukuliwa kaburi la Mlutheri aliyekosa urais. Kwani ni Walutheri waliomnyima huo urais? Watu 518 wanaongelewa utadhani ni maembe! Hata mmoja ni wengi.

TUJUTE NA KUOMBA RADHI. Walioua na waliouawa si Walutheri tu. Hata waliofanya maamuzi ya kuua siamini kama ni Walutheri. Achana na Ulutheri; Achana na Mlutheri. Tunagombanishwa na wamiliki wa bus sisi tukigombania seat! Rudi kwenye agenda ya nchi. Kero nyingi, watatuzi wachache. Tunatokaje hapa? Kwa kutekana?!

Wakurya wana msemo; “Anayebanja na kutema huwa anapunguza mzigo”.

Wajaluo hubanja na kumeza🤣🤣🤣
 
Kkkt ya Malasusa ni ya kimkakati , hata uwe mjinga kiasi gani lazima utambue hili
 
Machawa tu hao hakuna kitu......
Mchana kwenye mahubiri na makongamano wanawa-confort raia, usiku wanakutana na watawala kupanga yao
 
Duu uyuu mzee ukiongozwa na hisia ya kimudi mudi unaweza jua ameongelea dini kumbe waala
 
Huyu Askofu hajawahi kupungukiwa hekima wala ujasiri wa kuunena ukweli. Ukilinganisha falsafa ya huyu Askofu halafu ulinganishe ni zile takataka za Chand, ni ahera na jehanamu.
 
Back
Top Bottom