Askofu Bagonza: Wanaodhani wana furaha hawana furaha. Wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani hawana furaha

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
FURAHA KAENDA WAPI?

Waliopiga kura hawana furaha, Waliosusa/suswa hawana furaha. Waliopita bila kupingwa hawana furaha, Waliosimamia kura hawana furaha. Walioshinda hawana furaha, Walioshindwa hawana furaha

Waliopanga yaliyotokea hawana furaha, Waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha. Walioshauri hekima hawana furaha. Waliokaa kimya hawana furaha, Wanaounga mkono nilichoandika hapa, hawana furaha. Wanaopinga nilichoandika hapa, hawana furaha

Wanaodhani wana furaha hawana furaha, Wapinzani hawana furaha. Wapinzani wa wapinzani, hawana furaha. ILA wanaodhani hawana furaha, ni KWELI hawana furaha. Ni bora kujiuliza huyu furaha yuko wapi?
*****

Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Benson Bagonza ametaja makundi 14 ya watu anaodai hawana furaha kutokana na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini Tanzania uliofanyika jana Jumapili Novemba 24, 2019.

Askofu Bagonza ametoa andiko jipya leo Jumatatu Novemba 25, 2019, ikiwa ni siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa wagombea wa chama tawala CCCM wamepita bila kupingwa maeneo mengi.

Katika andiko lake hilo ambalo linasambaa katika mitandao ya kijamii ikiwamo makundi ya WhatsApp, Askofu Bagonza anasema waliopiga kura hawana furaha na waliosusa au kususwa hawana furaha.

Anasema waliopita bila kupingwa nao hawana furaha, waliosimamia kura hawana furaha, walioshinda hawana furaha na hata walioshindwa hawana pia furaha na uchaguzi huo

Katika andiko hilo, Askofu Bagonza anasema waliopanga yaliyotokea hawana furaha, waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha na walioshauri hekima hawana furaha.

Anasema kutokana na uchaguzi huo, waliokaa kimya hawana furaha, wanaounga mkono nilichoandika hapa hawana furaha na wanaopinga anachoandika hapa, hawana furaha.

“Wanaodhani wana furaha pia hawana furaha. wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani, hawana furaha. Wanaodhani hawana furaha ni kweli hawana furaha na kuhoji furaha yuko wapi,” anasema

Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika jana Jumapili huku vyama sita vya upinzani vikisusia uchagizi huo ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, UPDP, Chaumma na ACT- Wazalendo.

====
Michango ya wadau

 
Nilishawahi sema PHd ya Bagonza Ni feki .Huo utafiti wa wasio na furaha nchi nzima kaufanya wapi?

PhD kazi yake ni kushusha takwimu sio hisia au halucinations

Chuo gani kilimtunuku hiyo PhD? Anaongea Kama mlevi Hana takwimu hata moja veriafiable na reliable
 

Jiwe gizani.

Sisi PhD yake haituhusu tunaangalia kile anachokisema je kina ukweli?

Yule sio Pengo wala Nyaisonga.
 
Huyu si level yako. Haya uliyoandika kawaandikie wa level yako na si waelewa mkuu
 
Hiv nani mwenye furaha!?
Ule utafiti uliotolewa wa mwaka 2018 kuwa Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya sita toka mwisho kwa kukosa furaha duniani nadhani takwimu za sasa baada ya uchaguzi huu wa SM tutashindania nambari moja sisi na Afganistani. Na pengine tukawashinda kwa kishindo na kuwa taifa namba moja kwa ukosefu wa furaha.
Hapo hatuna vita, hatuna njaa wala majanga makubwa kama vimbunga,tetemeko au mafuriko, bali time"bahatika" kuwa na CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…