Askofu Bagonza: Wasemaji wengi wanasababisha wakosoaji wengi

Askofu Bagonza: Wasemaji wengi wanasababisha wakosoaji wengi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
DHAHABU: Wasemaji Wengi Wanasababisha Wakosoaji Wengi.
Tabia ya kufichaficha mambo, inasababisha serikali kujikanyaga na kutoa matamko yanayokinzana. “Matamko-mgongano” yakiwa mengi, yanasababisha wasemaji na wazushi wengi kama ilivyo sasa.

Ebu ona hili la kuuza RIZEVU/NYANTAKOLWAKOLWA yetu ya dhahabu ;

1. Mara Benki Kuu iseme “Reserve Haiuzwi” na kwamba watu wanazusha.

2. Baadaye inasema itauzwa kidogo tu iliyozidi. Na baadaye tena inasema itauzwa sehemu lakini si kulipia miundombinu.

3. Mtumishi mwingine wa Benki Kuu analiambia kundi la Whats up kwamba zitauzwa kulipia miradi ya Miundombinu lakini watanunua nyingine kwa sababu zipo!

4. Wizara ya Uwekezaji inanukuliwa na vyombo vya habari vya nje kuwa “Rais ameamua dhahabu ziuzwe kwa sababu bei ni nzuri kwa sasa”,

5. “Machawa wetu” huko bungeni wanasema dhahabu zitauzwa na muuzaji asisikilize maoni ya wananchi wanaoitwa wanaharakati.

6. Yote haya, hayakanushi ukweli kuwa AKIBA YA DHAHABU ITAUZWA. Dhahabu ni mali ya BOT; na BOT ni mali ya serikali; na serikali ni mali ya wananchi (hili sina uhakika sawasawa).
SASA

7. Mwaka jana liliibuka timbwili. Serikali ikauza “shares” zake za makaa ya mawe. Kampuni iliyonunua ikaziweka sokoni Australia. Mtanzania mmoja akaenda akazinunua. Sisi wenye fitna tukamrukia na kumwita majina yote mabaya. Alikosea wapi? Yaani unamwacha mke halafu hutaki aolewe tena?! Roho mbaya, Shingo feni.

8. Je, tukiuza akiba ya Dhahabu. Akatokea Mjaluo anayefanya kazi BOT. Akauza wake zake na kamongo wote ziwani, akazinunua; tukimjua tumsalie Novena au Albadir? Na huyo mtu akijikuta ana hazina ya dhahabu kubwa kuliko BOT, hatatuchagulia tulale na kuamka saa ngapi?

9. Uuzwaji huu wa RIZEVU ya dhahabu uliokuja ghafla kama hekima ya Wajaluo, ukija kugeuka kuwa KAGODA, IPTL, na Escrow nyingine, tuanze kuitana tumbili tena?

USHAURI WANGU:
a) Nenda pole pole. Haraka ya Bandari imetufikisha wapi?
b) Kuwe na Msemaji mmoja wa serikali. Kuwatumia wasanii kwa mambo nyeti ni kuidhalilisha serikali yetu hata kama inajifanya siyo yetu.
c) Bunge lijikite kuisimamia serikali siyo kuwasema wana harakati. Mishahara yao hailipwi kutoka mifuko binafsi ya wana harakati.
d) Ongeza uwazi. Dhahabu si madawa ya kulevya. Mambo ya siri na ya gizani, yalimsababisha Mjaluo amuoe kibogoyo aliyemposa gizani.
e) Kubali ukweli: Kwamba, kutikisa RISEVU yetu kutatikisa shilingi yetu. Msiposema na ikatikisika, tusianze kutekana tutakapoanza kuwazodoa. Tajiri asiye na RISEVU ni maskini kuliko maskini wa kipato mwenye RISEVU.
 
Pastor, umeshajitahidi sana kuwaamsha usingizini,ila wenyewe ni kama welevi walioelemewa kwa usingizi na ulevi kwa pamoja.Iwapo utaona inafaa wape muda watokwe na ulevi na kupungukiwa na usingizi halafu uwalishe madini haya mazito ambayo kwa hali yao ya sasa ni mazito mno kwao kuyahimili japo tu kujua wanapewa vitu vyenye samani kubwa kwao.
 
Haya mambo ni mazito kwa maslahi mapana ya taifa ntarudi nikitoka chimbo
Nikale kaya kwanza!
 
Socrates wa Tanzania. Na ikawa hivyo, vinginvyo hekima ya wajaluo ... itawafikia
 
Back
Top Bottom