Pre GE2025 Askofu Bagonza: Wizi na ulaghai kwenye uchaguzi utabomoa jina na heshima ya nchi

Pre GE2025 Askofu Bagonza: Wizi na ulaghai kwenye uchaguzi utabomoa jina na heshima ya nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Tunaikaribia Nigeria. Mambo haya yanaathiri utambulisho wa taifa letu. Baadhi yetu tumefaidi matunda ya jina zuri la taifa letu ndani na nje ya mipaka. Jina hilo lilijengwa kwa gharama kubwa na waasisi wa taifa letu. Popote ulipojitambulisha ni Mtanzania, watu waliinama kwa heshima kubwa.

Niliwasikia kwa masikio yangu baadhi ya viongozi wa sasa wa serikali yetu wakijiapiza kuwa “yakiyojitokeza katika awamu ya tano, yasiruhusiwe tena”.Rais Samia ana historia ya kujenga na tayari anayo. Ana Legacy ya kuacha, si kubebana na ya awamu ya tano.

CCM bado inao uwezo mkubwa wa kushinda chaguzi bila ulazima wa “kuonekana” inaiba kura. Naogopa kuamini kuwa sifa ya mwana CCM ni kuiba kura! Inatisha."

Soma: Askofu Bagonza: Madai ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yasimilikiwe na chama chochote
 
Back
Top Bottom