GE2025 Askofu Bagonza: Wote tuko njiapanda, Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reforms?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu, nawasogezea wino mzito wa Askofu Dkt. Benson Bagonza alioutumia kuwasilisha fikra tunduizi kupitia ukurasa wake Facebook

===

WOTE TUKO NJIAPANDA: Tupande gari gani?

Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA
 
Amen
 
Tatizo kubwa tulilo nalo, hivi kweli watawala wetu wana hekima ya kumwelewa mtu kama Askofu Bagonza?
Ukiwa na watawala waliokosa hekima na akili, kitu pekee wanachokitegemea huwa ni maguvu, na siyo busara wala akili.
 
PhD - Power higher Deeper Askofu 'amechimba' kina kirefu.
 
Back
Top Bottom