Askofu Bagonza: Yawezekana tulikuwa na Bunge bila Spika. Tunakoelekea tunaweza kuwa na Spika bila bunge

Askofu Bagonza: Yawezekana tulikuwa na Bunge bila Spika. Tunakoelekea tunaweza kuwa na Spika bila bunge

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
MAMA TUVUSHE, TUKUVUSHE

Yawezekana tulikuwa na Bunge bila Spika. Tunakoelekea tunaweza kuwa na Spika bila bunge. Bila ushabiki wala uzembe, tuangalie yafuatayo kwa makini:

1. Ukubwa wa CCM si mtaji, ni hatari. Bila upinzani imara, CCM ni sawa na chatu aliyefugwa ndani chungu cha mfinyanzi. Akikosa chakula atamla mfugaji.

2. Mihimili mitatu ya kufikirika ni hatari kwa nchi. Mmoja juu ya mingine ni kitanzi cha amani yetu.Tatizo Wanaofunikwa wanapenda.

3. Isiwe sheria wakuu wa mihimili kualikana kila wakati na kila mahali. Tunadhoofisha uadilifu wa mihimili yote. Kujipendekeza kumestawishwa kupitia huko.

4. Tuharamishe kujipendekeza kama tulivyoharamisha kukashifu Viongozi.

5. Mgombea binafsi anaweza kuwa Spika mzuri ili kuokoa uadilifu wa bunge. Kama mahakama isivyo na mahakimu/majaji wenye vyama na Spika asiwe na chama.

6. Afya ya Taifa ni mshikamano wa dini mbalimbali, makabila, jinsia, na itikadi mbalimbali. Mshindi anayechukua vyote ni sumu kwa amani yetu. Bora upinzani wa nje kuliko wa ndani.

7. Mjadala wa Haja ya kuwa na Katiba Mpya usitishwe. Huu ni wakati wa kutekeleza si kujadili.

8. Tangu uhuru tumetawaliwa na chama kimoja awamu tofauti. Kila awamu ina mambo yake. Zipo zilizotawanya na kurarua. Namlilia Mungu ili hii ya (6 au ya 5) iwe ya kuunganisha na kuponya majeraha. Anayesita zamu yake yaja.

9. Sakata la Ndugai (Ndugaigate) limefunua aibu yetu. Mfumo dume uko imara lakini pia bibi mwenye ndizi mbivu hakosi wajukuu wa kutuma mtoni. Waliojituma hongera, mliotumwa kuna siku mtatumwa kutafuta vitanzi vyenu.

10. MUNGU YUPO na ANATUONA. Si kila kitu tulichofanya 2020 kilibarikiwa na Mungu! Tukubali aturekebishe kwa sababu tumemtaja sana tangu 2020 na tumeshika misahafu tukaapa kwa jina lake. ZINGATIA HILI: Pasipo na haki huwa hayupo.

MAMA TUVUSHE ILI TUKUVUSHE. Kama una mashaka, Kuna MWAMBA mzoefu wa kuvusha, anaweza kusaidia.
 
7. Mjadala wa Haja ya kuwa na Katiba Mpya usitishwe. Huu ni wakati wa kutekeleza si kujadili.
Nimeipenda sana hii. Kama kuna mtu bado anabisha zamu yake ya kusema majuto ni mjukuu inakuja
 
NANI ALIJUA?
Acha Mungu aitwe MUNGU.[emoji19][emoji19][emoji19].
Screenshot_20220107-094833.jpg
 
Sakata la Ndugai (Ndugaigate) limefunua aibu yetu. Mfumo dume uko imara lakini pia bibi mwenye ndizi mbivu hakosi wajukuu wa kutuma mtoni. Waliojituma hongera, mliotumwa kuna siku mtatumwa kutafuta vitanzi vyenu.
...mwenye masikio ameshasikia..na mwenye kujua kusoma ameshasoma.
 
Nimeipenda sana hii. Kama kuna mtu bado anabisha zamu yake ya kusema majuto ni mjukuu inakuja
... kwa Katiba hii, hakuna aliye salama hata Mama baada ya kuondoka madarakani hatakuwa na usalama siku "mwehu" akikamata madaraka kwa Katiba hii inayotoa mamlaka ya kiungu kwa mtawala! Katiba hii ni hatari mno kwa usalama wa taifa hususan kadiri makundi yanavyozidi kujiunda na kumea! Wenye busara na wastuke no matter wana itikadi gani.
 
...Walioshika madaraka hawataki kuisikia hiyo katiba mpya ndio maana kuna kiongozi wa upinzani amepewa kesi ya mchongo ya 'ugaidi' baada ya kuidai hiyo katiba.
 
...Walioshika madaraka hawataki kuisikia hiyo katiba mpya ndio maana kuna kiongozi wa upinzani amepewa kesi ya mchongo ya 'ugaidi' baada ya kuidai hiyo katiba.
... sawa ila waombe Mungu waendelee kutawala wao; wasije wakajichanganya wakampa nafasi "mwehu" ataingiza taifa matatizoni. Tutaumia wote!
 
"......bibi mwenye ndizi mbivu hakosi wajukuu wa kutuma mtoni. Waliojituma hongera, mliotumwa kuna siku mtatumwa kutafuta vitanzi vyenu........"
 
Kina Lema na wafuasi wao wanashangilia kama mazuzu bila kujua kama bunge ndio limepigwa nyundo mazima!

[emoji23][emoji23][emoji23]Nchi hii mataahira yapo kila kona
 
... sawa ila waombe Mungu waendelee kutawala wao; wasije wakajichanganya wakampa nafasi "mwehu" ataingiza taifa matatizoni. Tutaumia wote!
...Wana uhakika wa kuendelea kutawala miaka mingi ijayo.....kuhusu kujichanganya inaweza kutokea maana hata wao ni binadamu.
 
Happy sijaelewa:
Usitishwe= usimamishwe?
Au
Usitishwe= kusiwe na kitisho dhidi ya?
.... kaeleweka vizuri tu. Anamaanisha Katiba Mpya ni suala la dharura kwa sasa sio tena suala la mjadala wa haja (sababu/umuhimu) ya kuwa (au kutokuwa) na Katiba Mpya bali kinachotakiwa (kwa hali iliyopo sasa) ni UTEKELEZAJI wa kuanzisha Katiba Mpya.
 
Happy sijaelewa:
Usitishwe= usimamishwe?
Au
Usitishwe= kusiwe na kitisho dhidi ya?
Nadhani ana maana tusitishe kuendelea kujadili na badala yake tuanze kutekeleza upatikanaji wa hiyo katiba mpya. Tumejadili sana. Haja ya kuwa na katiba mpya siyo mjadala tena.
 
Back
Top Bottom