Askofu Benson Bagonza: Tumeamua kumuomba Mungu kama Taifa, kweli tumuombe Mungu na siyo kumtukuza au kumsifia mwanadamu yeyote

Watu wengi hatujui hata namna ya kuombea Taifa lipate uponyaji.....

Badala ya kuomba unaanza kusema " kama alivyosema mtukufu Rais...."

Hayo yatakuwa si maombi tena....
 
Ukiwa na njaa, utakuwa mjinga kukaa chini na kusema unamwomba Mungu akushibishe njaa yako. Wanaolijua neno wanaenda kufanya kazi na kuomba baraka ya kile anachokifanya ili kimpe shibe.
 
Nilijua una muongelea "Mungu", kama ni "mungu" hata mimi nakuunga mkono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah... Moderator, naona post yangu imechakachuliwa kiaina.
haya bana!
 
soma Hosea 4:6
 
Huyu Dk. Bagonza na Niwemugizi ni wivu tu dhidi ya Jiwe ndio unawasumbua.
Toka kale, manabii na mitume wakweli, mara nyingi walikuwa kinyume cha watawala kwa sababu watawala hutafuta utukufu wakati anayetakiwa kutukuzwa ni Mungu.

Ni watawala ndio walimhukumu Kristo Masiha. Ni watawala waliowafunga na kuwanyonga mitume. Watu wa Mungu wautafute ukaribu na Mungu na wala siyo watawala.

Watawala wanaomjua Mungu, nao huutafuta ukaribu na Mungu, siyo na majeshi au wasiojulikana.
 
Umeongeza umbea kwenye maneno ya Bagonza!
 
Tatizo fedha zinazochangwa kama kawaida hazijulikani zinatumikaje lkn cha ajabu watu bado wanahimizwa kuchanga tu.

Kando ya kwamba fedha zilizolenga kutumika kwenye sherehe ya muungano na za kukimbiza mwenge pia ziliamuliwa zitumike kwenye hili janga.

Tatizo kubwa tulilonalo leo ktk nchi hii ni kuwa hakuna uwazi ktk matumizi ya fedha za serikali na ktk maeneo fulani fulani hakuna ukaguzi unaoruhusiwa kufanyika jumbo linalodhihirisha kwamba uwezekano wa ubadhirifu ni mkubwa sana.
 
Kuna comedy film moja ya Chris Rock, Head of State, mgombea mmoja wa Urais alikuwa anamalizia hotuba zake kwa kusema, “God Bless America, and no place else”. Ndiyo tulipofikia sasa Tanzania.
 
Hakuna mtu anayepewa sifa na kutukuzwa, bali kinachofanyika ni "mnyonge mnyongeni lakin haki yake mpeni kama vile tufanyavyo kwa viongozi wengi wetu wa dini ikiwamo na kwa akina POPE wetu. Tunawapa heshima yao kama watumishi wa Mungu na kuwasifia pale wanapo tuongoza vizuri au siyo Askofu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…