Besta Mlagila
Senior Member
- May 29, 2018
- 101
- 191
Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo ameonya wale wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuandika mambo machafu na kutukana wengine kuwa wanahatarisha amani ya nchi.
Askofu Cheyo amesema hayo, Jumatano Desemba 25,2019 wakati akitoa salamu za Krismasi katika ibada la Kanisa la Moravian Viwawa mjini Wilayani Mbozi mkoani Songwe kuwa amani na umoja wa nchi unapaswa kulindwa na kila mmoja ili watu waweze kufanya kazi ya kujiletea maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla.
Alisema "Wapo wenzetu ambao wanatumia vibaya elimu na uhuru wa habari kuharibu amani yetu, aidha kwa kutumika na watu wasioitakia mema nchi yetu na hao nawaambia nchi hii ndiyo tuliyopewa na Mungu tunapaswa kuilinda," amesema Askofu Cheyo.
Askofu Cheyo ametumia pia nafasi hiyo kutuma salamu za kumtakia heri Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kazi njema ya kuliongoza Taifa hili