Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.
Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;
1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.
2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.
3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.
4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.
Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.
Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.
Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!