Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza ametoa wito kwa Watanzania hususani wanasiasa kutafakari mustakabali wa Taifa ulivyo, akidai kuwa endapo mambo yatabaki kama ilivyo sasa huenda 'kama Taifa' tukaelekea kubaya zaidi kutokana na mgawanyiko uliopo sasa hapa nchini
Akihojiwa na Jambo TV, muda mfupi baada ya kukamilika kwa ibada ya faraja ya kuaga mwili wa Askofu (mstf) Dkt. Stephen Munga iliyofanyika leo, Jumanne Septemba 23.2025 kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Kunduchi Beach, Dar es Salaam, amesema kuwa hatua tuliyofikia sasa kama Taifa ya kuwepo kwa taarifa za matukio ya utakaji, mauaji nk haileti taswira nzuri kwenye 'jicho' la umoja na mshikamano
Akizungumzia Askofu (mstf) Dkt. Stephen Munga aliyefariki Jumamosi ya Septemba 20.2025, akitarajiwa kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele kesho, Jumatano Septemba 24.2025 huko mkoani Tanga, Askofu Dkt. Bagonza amemtaja kama miongoni mwa watu waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania haki, kusimamia kile anachokiamini kama tu kinalenga kunufaisha jamii.