Askofu Dkt. Mwaikali wa Konde KKKT aangukia pua mahakamani!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594

Askofu Dr Edward Mwaikali ambaye baada ya mkanganyiko mkubwa katika Dayosisi ya KKKT-Konde alifungua shauri mahakama Kuu Mbeya kupinga kuenguliwa Uaskofu, sasa rasmi Mahakama imeamua kuwa haina mamlaka kuzuia kuapishwa Askofu Geofrey Mwakihaba, ambaye alichagulikwa na Mkutamo Mkuu wa Dayosisi hivi karibuni.

Ujumbe kwa aliyekuwa Askofu Dr Edward Mwaikali, waswahili wepesi tu walisema , asiyesikia la mkuu, huvunjika guu, na heshima yake.

Ref: Toka kwa rafiki yangu Mwakipalule-Syanaloli,

cc https://www.jamiiforums.com/members/masopakyindi.47580/
 
Kutoka kwa Mwenegoha mpaka leo Mwaikali,KKKT halijawahi kutulia na haitakaa itulie. Utaratibu wa kuwapata maaskofu kwa kura nadhani unatakiwa utafakariwe.
Wasipopatikana kwa njia ya kura, ulitaka maaskofu wa KKKT wapatikane kwa njia gani itakayokuwa bora?
Wateuliwe? Na nani? Itakuwa njia bora?
 
Askofu Dr Edward Mwaikali ambaye baada ya mkanganyiko mkubwa katika Dayosisi ya KKKT-Konde alifungua shauri mahakama Kuu Mbeya kupinga kuenguliwa Uaskofu, sasa rasmi Mahakama imeamua kuwa haina mamlaka kuzuia kuapishwa Askofu Geofrey Mwakihaba, ambaye alichagulikwa na Mkutamo Mkuu wa Dayosisi hivi karibuni.

Ujumbe kwa aliyekuwa Askofu Dr Edward Mwaikali, waswahili wepesi tu walisema , asiyesikia la mkuu, huvunjika guu, na heshima yake.

Ref: Toka kwa rafiki yangu Mwakipalule-Syanaloli,
cc https://www.jamiiforums.com/members/masopakyindi.47580/

Kwa kweli tabia ya huyu Askofu Mwaikali ametutia aibu sana wanyakyusa.
Haonyeshi tabia asili tulizo nazo ambazo ni kusimamia ukweli na kutokuwa na roho ya kifisadi na kupenda kumtumikia Mungu kwa roho na kweli.
Sasa anaaibika mbele ya mbingu na ardhi.
 
Ya kanisa gani ? Wakati akina Mwandosya wanamuomba asihamishe makao makuu ya Dayosisi Kibabe aliwapuuza , kiko wapi sasa ?
Niliiona ile clip Prof Mwandosya alipomuonya na kumpa nasaha kama mtu mzima.
Asiyesikia la mkuu keshavunjika mguu!
 
Wasipopatikana kwa njia ya kura, ulitaka maaskofu wa KKKT wapatikane kwa njia gani itakayokuwa bora?
Wateuliwe? Na nani? Itakuwa njia bora?
RC wanapatikanaje? Ulishasikia wamepelekana mahakamani? Hii ya KKKT na Anglikan litaendelea kuwa tatizo tu leo Mokiwa kesho Malasusa ni makundi tu kila unapofika uchaguzi wa askofu au Dean.
 
Hili dhehebu lijitafakari sana.Mahakama ya kidunia inatumika kusuluhisha mambo ya kiroho ya waumini? Yaani mahakama inatoa Hatma ya maisha ya kiroho ya waumini? Inasikitisha sana.
 
Mimi Mluteri.
Naona hili tatizo la Mwaikali limepigwa chini mahakamani baada ya kupelekwa huko na huyo Askofu.
Waumini hawakulipeleka shauri mahakamani.
 
Hili dhehebu lijitafakari sana.Mahakama ya kidunia inatumika kusuluhisha mambo ya kiroho ya waumini? Yaani mahakama inatoa Hatma ya maisha ya kiroho ya waumini? Inasikitisha sana.
Hata hiyo Mamlaka imewekwa/imeruhusiwa kuwapo na Mungu

Kwani utawala wa Misri uliokuwa unawahumu kwa mateso Waisrael haukuwekwa au kuruhusiwa kuwapo na Mungu?
 
Back
Top Bottom