Askofu Dkt. Mwaikali wa Konde KKKT aangukia pua mahakamani!

Askofu Dkt. Mwaikali wa Konde KKKT aangukia pua mahakamani!

Hili dhehebu lijitafakari sana.Mahakama ya kidunia inatumika kusuluhisha mambo ya kiroho ya waumini? Yaani mahakama inatoa Hatma ya maisha ya kiroho ya waumini? Inasikitisha sana.
Mbona mgumu kuelewa mkuu.
Kanisa halikupeleka shauri mahakamani ila ni huyo askofu aliyepotoka ndiye kapeleka shauri mahakamani.

Mahakama imemkana kuwa haihusiki na mambo ya kuendesha kanisa na taratibu zake.
Ameambiwa arudi huko au akate rufaa.
 


Askofu Dr Edward Mwaikali ambaye baada ya mkanganyiko mkubwa katika Dayosisi ya KKKT-Konde alifungua shauri mahakama Kuu Mbeya kupinga kuenguliwa Uaskofu, sasa rasmi Mahakama imeamua kuwa haina mamlaka kuzuia kuapishwa Askofu Geofrey Mwakihaba, ambaye alichagulikwa na Mkutamo Mkuu wa Dayosisi hivi karibuni.

Ujumbe kwa aliyekuwa Askofu Dr Edward Mwaikali, waswahili wepesi tu walisema , asiyesikia la mkuu, huvunjika guu, na heshima yake.

Ref: Toka kwa rafiki yangu Mwakipalule-Syanaloli,
cc https://www.jamiiforums.com/members/masopakyindi.47580/

mambo ya imani sasa hadi mahakamani?
 
Back
Top Bottom