MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Askofu Dk. Fredrick Shoo amewaomba watu wote wanaojua kuomba waungane kumuomba Mungu ili yale yanayotendeka hapa nchini yatendeke Kwa haki na si Kwa kuonea watu.
Akizungumza katika ibada ya mazishi ya kumpumzisha mke wa Edwin Mtei, Johara Mtei nyumbani kwake Tengeru wilayani Arumeru, Dk. Shoo alitoa pole kwa mke wa Mbowe Lilian Mbowe Kwa kuondolewa na mama yake na kumtaka ajipe moyo hasa katika kipindi hiki ambacho mumewe ameshindwa kumzika mama mkwe wake sababu ya kesi ya ugaidi.
"Najua shauri la Mbowe lipo mahakamani naomba sana wale ambao wamepewa dhamana ya kutoa haki wakatende yake ambayo ni mapenzi ya mungu na haki ikasimame"alisema Askofu
Askofu Shoo alisema anashangaa kusikia Mbowe anashtakiwa Kwa ugaidi kwani Kuna wakati walipanga maandamano ya Ukuta viongozi wa dini walimwita Mbowe na kumshauri asiende barabarani Kwa kuwa damu za watu zitamwagika Jambo ambalo Mbowe alikubali kwa unyenyekevu kwa kusema hatapenda kuona damu za watu zikimwagika.
"Nitashangaa kama mbowe amebadilika na kuwa gaidi namfahamu Mbowe nikiwa Askofu wake na Mbunge wangu Jimbo la Hai, hakuwa na tabia hiyo naomba haki ituongoze, uzuie ulimi wako na mabaya, mambo ya kusingizia wengine ni mbaya Sana"alisema Dr Shoo
"Kibinadamu yanaumiza ukiona yanayotendeka mambo ya ajabu nchini maana Freeman Mbowe ameshindwa kumzika baba mdogo wake na mama mkwe hakika sisi tunaofuatilia mambo haya yanaumiza kibinadamu,"alisema
Alisema wale wanaoonewa ipo siku watamlilia mungu na sauti zao zitasikika na mungu atajibu maombi yao
"Ukiwa na mamlaka yoyote yatumie kwa kutenda haki na tuangalie yale tunayosema kweli na haki ,tusisingiziane uwongo,"alisema
Aidha alisema shauri la Mbowe lipo mahakamani hivyo aliomba wale wote waliopewa dhamana ya kutrnda haki wakatende haki na haki ikasimame.
Alisema mambo magumu na mazito ya kusingiziana vema yakazuiwa na kila mtu kupitia ndimi zao.
"Wapo watu mioyo yao inaugua hata bila kuwa na sehemu ya kusemea hivyo ili ipone lazima haki itendeke,sababu hata ukimuuliza kipofu hapa kuna haki yoyote inasikitisha,"alisema
Alisema pamoja watu wanasema siasa mchezo mchafu lakini vema watu wasifanye kupitiliza kwa sababu wapo watu watamlilia mungu na atajibu.
Aliomba watu watafute kufanya siasa za kistaarabu na kukaa katika maridhiano ambalo ndilo ombi lao siku zote.
Alimalizia kusema nchi ili ifanikiwe nilazima iweze kutenda haki sababu wapo watu wanaomba pale haki inapotoweka na Mungu hujibu.